Klabu Bingwa Afrika: Dar Young African Vs Zesco

Kwani kule kwa Townshipp Rollers tulipewa Penalti?
Shadeeya mamii usilinganishe kiwango cha Makhirikhiri na Zambia, Zambia li level ingine bana
Kwa hili nionavyo tunywe Mtori nyama tutazikuta chini kwani bahati ya kuzilenga nyavu tu ndio hatuna lakini hizo move tunazitengeneza sana tu.
Kwahiyo bado unaamini kwenye soka la sasa kuna kitu bahati? Ukizidiwa umezidiwa mkubali tu na kama mtu anajua anajua tu wala msisingizie bahati
Haya ni mawazo yenu tu love na wala hatuchezi mpira tukiyatarajia hayo. Na pia niseme ile ni sehemu ya mpira hivyo yote tumeyapokea na kujipanga kwa 90 mins za kule Zambia ambazo nina hakika tutazitumia vyema. 😎
Nawasubiria kwa hamu niwaone mtakavyozitumia vyema dk 90 za huko Zambia kupunguza magoli mtayopachikwa 🤣 🤣 🤣
 
Hahahaaa uzuri wa Yanga ni hapo tu, mna roho saba nyie, yaani mnaona mnaenda kufa hivihivii lakini bado mnajipa moyo tu
Hatuezi jiweka huko wakati game ya kwanza mlijua hatuna chetu na mwisho wa siku tukawaduwaza.

Hivyo bado nina imani na timu ya Wananchi ses tukishakufa ndio tutazungumza mengine ila kwa sasa naona nafasi bado tunayo.
 
Shadeeya mamii usilinganishe kiwango cha Makhirikhiri na Zambia, Zambia li level ingine bana
Haya tutayajua Septemba 28 Ses na hapo ndio utakuwa wasaa mzuri wa kulinganisha
Kwahiyo bado unaamini kwenye soka la sasa kuna kitu bahati? Ukizidiwa umezidiwa mkubali tu na kama mtu anajua anajua tu wala msisingizie bahati
Hii kauli muliitumia mlipotolewa na Du Songo kwamba hamkuwa na bahati lakini leo unasema hakuna bahati kwenye mpira. 😀😀😀
Nawasubiria kwa hamu niwaone mtakavyozitumia vyema dk 90 za huko Zambia kupunguza magoli mtayopachikwa 🤣 🤣 🤣
Lets wait and see kipenzi.
 
Hatuezi jiweka huko wakati game ya kwanza mlijua hatuna chetu na mwisho wa siku tukawaduwaza.

Hivyo bado nina imani na timu ya Wananchi ses tukishakufa ndio tutazungumza mengine ila kwa sasa naona nafasi bado tunayo.
Tusiandike mate na wino ungalipo Shadeeya
 
Haya tutayajua Septemba 28 Ses na hapo ndio utakuwa wasaa mzuri wa kulinganisha
Tuombe uzima yetu macho Shadeeya
Hii kauli muliitumia mlipotolewa na Du Songo kwamba hamkuwa na bahati lakini leo unasema hakuna bahati kwenye mpira. 😀😀😀
Wale Wamakonde hawakutuzidi kwa lolote sema sisi tuliwadharau ndio kilichotuponza, ila nyie mmemaliza mbinu na gea zote, ndio kiwango chenu kilipoishia ujue
Lets wait and see kipenzi
Haya love daktari wako wa pressure ntakuwepo kukupa kuanzia huduma ya kwanza hadi tiba yenyewe kamili mamii
 
Tuombe uzima yetu macho Shadeeya
Hakika
Wale Wamakonde hawakutuzidi kwa lolote sema sisi tuliwadharau ndio kilichotuponza, ila nyie mmemaliza mbinu na gea zote, ndio kiwango chenu kilipoishia ujue
Haya ni yenu nguvu moja kwamba kiwango chetu kimeishia pale.
Haya love daktari wako wa pressure ntakuwepo kukupa kuanzia huduma ya kwanza hadi tiba yenyewe kamili mamii
Hahahaaa. Mwisho wa siku kibao kisije geuka tu mie ndio nikawa Daktari tu. 🙈🙈🙈
 
Hivi kwanza ilikuaje mkamuachia Kamusoko aondoke mpaka sasa anakuja kuwaadhirisha nyumbani? Maana lile shuti alipiga kwa hasira sana, sijui alikua ana mawzo gani kichwani mwake dhidi ya Chura FC
 
Back
Top Bottom