KKKT: Kikwete usiwaweke viporo Mafisadi

KKKT: Kikwete usiwaweke viporo Mafisadi

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
58,063
Reaction score
134,408
Katika ibada ya jumapili ya leo huku Moshi Askofu wa KKKT Dr.Fredric Shoo amemtaka Rais Kikwete na serikali ya CCM wasiwaweke viporo mafisadi.Akihutubia waumini wa dhehebu hilo Dr.Shoo amemtaka rais kuacha kulea watu wachafu ndani ya utendaji wake. Katika misa hiyo walihudhuria pia Dr. Alex Malasusa,Mh.Mbowe,Lowasa na Dr.Mengi.Aidha Dr.Malasusa amesisitiza kuwa amani ni zao la haki,kwamba ili amani izidi kutamalaki ni lazima serikali itende haki kwa watu wake
 
Kikwete sikio la kufu tusubiri tuona hatma Ya hii SERIKALI dhalim
 
Katika ibada ya jumapili ya leo huku Moshi Askofu wa KKKT Dr.Fredric Shoo amemtaka Rais Kikwete na serikali ya CCM wasiwaweke viporo mafisadi.Akihutubia waumini wa dhehebu hilo Dr.Shoo amemtaka rais kuacha kulea watu wachafu ndani ya utendaji wake. Katika misa hiyo walihudhuria pia Dr. Alex Malasusa,Mh.Mbowe,Lowasa na Dr.Mengi.Aidha Dr.Malasusa amesisitiza kuwa amani ni zao la haki.

mimi ni mkristo. na katika ukristo uongo,wizi n.k havitakiwi. mda mwingine viongozi wa dini ni madalali na wahusika wakuu wa kupoteza waumini wao. wao wenyewe ndio wanawakumbatia hao anaomwambia fastjest asiwaweke kiporo
 
inashangaza kuona kiongozi mkuu analinda majambazi wa fedha za umma,eti naye anadai sio za umma.tulikuchagua uwatete watanzania sio unatetea IPTL na mafisadi wa escrow.IPTL hawakukupigia kura?
 
Kikwete sikio la kufu tusubiri tuona hatma Ya hii SERIKALI dhalim

Hiki ulichosema ni sahihi kabisa. Sikio la kufa halisikii dawa. Mimi nina mfano hai kuhusu sikio la kufa kutosikia dawa. Mimi ninamshikaji wangu alikuwa masomoni nje ya nchi kwa muda wa miaka minne. (Wakati anaenda masomoni alikuwa mwajiriwa wa serikali hii ya mshikaji). baada ya kuondoka tu kama miezi miwili Mwajiri akaanza kutumbua mshahara wake. Mshahara alikuwa amewaachia familia yake, hivyo familia walivyoenda kuangalia hawajakuta kitu wakampa taarifa, Kawasiliana na Mhasibu kazini kwake mhasibu kamwambia boss kasema tusimamishe kukulipa. Kumbe mshahara unatoka boss anafanyia starehe. Jamaa alivyokuja likizo akamface boss kutaka kujua boss ana mpiga chenga. Kwa kuwa alikuwa na scholarship awa anadunduliza hivyo vipesa vya scholarship kula yeye na kusaidia familia. Alivyo maliza shule yake karudi kazini kumwambia boss ana mjibu ovyo. (mimi ni Kikwete ni Mshikaji wangu) huwezi kunifanya chochote. (na kweli Kikwete alikuwa mshikaji wake). Basi mshikaji kapiga chini kwa chini. Mbona Boss alistukia analetewa barua ya kustaafishwa kwa manufaa ya umma. Sasa hivi huko mtaani anapiga watu mizinga tu. Kwa hiyo hata kikwete anaweza kuwa anasema hakuna lolote, siku yakitokea ndo najuta.
 
mimi ni mkristo. na katika ukristo uongo,wizi n.k havitakiwi. mda mwingine viongozi wa dini ni madalali na wahusika wakuu wa kupoteza waumini wao. wao wenyewe ndio wanawakumbatia hao anaomwambia fastjest asiwaweke kiporo

kweli unaonambali ,umeona jinsi askofu kilaini alivyojijazia minoti ya umma halafu anajiita mcha mungu.anaombea maskini huku anawafyonza viutomvu vya uhai.
 
Katika ibada ya jumapili ya leo huku Moshi Askofu wa KKKT Dr.Fredric Shoo amemtaka Rais Kikwete na serikali ya CCM wasiwaweke viporo mafisadi.Akihutubia waumini wa dhehebu hilo Dr.Shoo amemtaka rais kuacha kulea watu wachafu ndani ya utendaji wake. Katika misa hiyo walihudhuria pia Dr. Alex Malasusa,Mh.Mbowe,Lowasa na Dr.Mengi.Aidha Dr.Malasusa amesisitiza kuwa amani ni zao la haki,kwamba ili amani izidi kutamalaki ni lazima serikali itende haki kwa watu wake

Wezi watafanya hila watawatuma baadhi ya vibaraka utasikia wanakuja na hoja dhaifu kuwa huo ni mfumo krt
 
Hilo la kiporo,Mh.Prof. Aliangalie lisije kuchacha
 
Kanisani watu ibada siku hizi ni kuzungumzia serikali na kutoa amri. Mungu wa wakristo yupo kwenye mikono ya wanasiasa.
 
hivi huko mkanisani wanahubiri nini? hebu imulikeni hii list Dr. Alex Malasusa,Mh.Mbowe,Lowasa na Dr.Mengi.
Eti amani ni zao la haki!!!! sijui wananongelea haki ipi wakati wanadhulumu na kuiibia serikali kila siku. kwenye escrow waliiba kuanzia viongozi, waumini mpaka na benki yao, kama wamechukua hela kutoka kwenye parokia au kigango. ovyo kabisa.

Katika ibada ya jumapili ya leo huku Moshi Askofu wa KKKT Dr.Fredric Shoo amemtaka Rais Kikwete na serikali ya CCM wasiwaweke viporo mafisadi.Akihutubia waumini wa dhehebu hilo Dr.Shoo amemtaka rais kuacha kulea watu wachafu ndani ya utendaji wake. Katika misa hiyo walihudhuria pia Dr. Alex Malasusa,Mh.Mbowe,Lowasa na Dr.Mengi.Aidha Dr.Malasusa amesisitiza kuwa amani ni zao la haki,kwamba ili amani izidi kutamalaki ni lazima serikali itende haki kwa watu wake
 
si huyu huyu mkuu wa kaya pale dodoma sakata la richmond alisema haijui dowans wala wamiliki wake! inatia shaka kumkabidhi nchi mtu asiyeweza hata kujitambua!
 
si huyu huyu mkuu wa kaya pale dodoma sakata la richmond alisema haijui dowans wala wamiliki wake! inatia shaka kumkabidhi nchi mtu asiyeweza hata kujitambua!
kwa wale wanaosifia mtu mwenye maamuzi magumu, kikwete naye ana maamuzi magumu sana mpaka watu kushindwa kumwelewa. kutokutoa uaamuzi kwenye issue nyeti/sensitive nayo ni uamuzi mgumu. Iddi amin alikuwa na maamuzi magumu, vichaa nao wa maamuzi magumu, kuvamia nchi na kunyang'anya kipande cha nchi nyingine kama alivyofanya Putin huko Ukraine ni maamuzi magumu na sasa nasikia Lowasa naye ana maamuzi magumu ya kwenda kutafuta artificial rain huko Asia au kumtishia mtoto aliyeuliza kwanini viongozi wana vyeo zaidi kimoja. mtu angesifiwa kuwa ana maamuzi sahihi anafaa kuwa raisi ningewalewa. lakini wanasema jamaa ana maamuzi magumu ni kuchunga sana maana hata vichaa wa maamuzi magumu.
 
Katika ibada ya jumapili ya leo huku Moshi Askofu wa KKKT Dr.Fredric Shoo amemtaka Rais Kikwete na serikali ya CCM wasiwaweke viporo mafisadi.Akihutubia waumini wa dhehebu hilo Dr.Shoo amemtaka rais kuacha kulea watu wachafu ndani ya utendaji wake. Katika misa hiyo walihudhuria pia Dr. Alex Malasusa,Mh.Mbowe,Lowasa na Dr.Mengi.Aidha Dr.Malasusa amesisitiza kuwa amani ni zao la haki,kwamba ili amani izidi kutamalaki ni lazima serikali itende haki kwa watu wake

Hiyo misa imewakilisha mawazo ya Mengi , yaani Mengi sasa kaona akina Sendeka wamekula Mapesa yake pasipo Muhongo kung'oka kaamua kuhamia makanisani tena kaanzia kwao Moshi, Mengi Safari hii utachunwa sana na bado Muhongo anadunda tu.
 
Wajinga kama hawa kwa jk watashuka tu sijawahi kuona jk anatishiwa nyau na wahuni na mafisadi kama hawa chapa kazi jk pamoja na muhongo kiboko ya mafisadi.
 
hivi huko mkanisani wanahubiri nini? hebu imulikeni hii list Dr. Alex Malasusa,Mh.Mbowe,Lowasa na Dr.Mengi.
Eti amani ni zao la haki!!!! sijui wananongelea haki ipi wakati wanadhulumu na kuiibia serikali kila siku. kwenye escrow waliiba kuanzia viongozi, waumini mpaka na benki yao, kama wamechukua hela kutoka kwenye parokia au kigango. ovyo kabisa.

Mengi ni Fisadi number one na maasikofu nao ni mafisadi siku hizi hakuna mtu wa kumwamini hata Mengi Mwenyewe kapigwa Pesa na Akina Sendeka na Abdul Mtegeta na wameshindwa kumng'oa Muhongo, huo pia ni Ufisadi wa ndani kwa ndani, Mengi ni Fisadi lakini na yeye kufanyiwa Ufisadi na akina Sendeka, yaani ni piga nikupige.
 
Wajinga kama hawa kwa jk watashuka tu sijawahi kuona jk anatishiwa nyau na wahuni na mafisadi kama hawa chapa kazi jk pamoja na muhongo kiboko ya mafisadi.

Eti misa iliendeshwa na Mtu anaitwa Dr shoo kisha Dr Mengi alikuwemo ndani ! Unategemea nini? Yaani Chuki ya Mengi juu ya Muhongo kaipenyeza hadi kanisani ! Mengi mwenyewe kaoa mjuukuu wake kazaa naye mapacha pasipo kuvunja ndoa ya awali kisha afunge ndoa rasmi huko kanisani anafuata nini wakati si msaafi.
 
Mengi + Mkono gawanya kwa Sendeka,kafulila, zito, Mnyika na sasa makanisani = Muhongo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom