KKKT (ELCT) Recycles Malasusa

nimeshangaa sana kujua kwamba Malasusa aligombea tena alafu wakampa. 2019 hivyo hivyo aligombea tena wakati alishakuwa mkuu wa kanisa. Huyu mtu theolojia anaijua lakini kazi ya uchungaji kama vile kwake sio ya wito.

Baba askofu Bagonza au pengine huyo wa Makete ingawa simjui ingekuwa safi sana kwa kanisa na kwa nchi kwa ujumla.
 
Unampa vipi hongera huyo muhuni?
Kwan huyu askofu kapigiwa kura na Akina nani, maana anashutumiwa Sana, pengine walio mpigia kura ndio wahuni wabobezi,
AU nao kkkT wanaiba kura kama NEC,

Malasusa Sio muhuni pekee, kkkT Kuna wahuni wengi sana yan
 
Tatizo ni kwamba watu wanawaza kila jambo kisiasasiasa kwa hiyo hata kama kitu sio watajaribu kuunganisha doti mpaka anaweza fikiri ni kweli. Kwa mpaka mtu anachagulia Mara ya pili katika mazingira kama haya ya vipindi viwili tofauti wajumbe walichambua in out ya wote na kuonelea Mwalasusa ashike kijiti tena hizi ni taasisi nyeti hazi hitaji mihemuko katika kufanya maamuzi
 
Nionavyo mimi hamkufurahishwa na Dr.Malasusa kabisa. Jaribuni kuvumilia tu kule hawakati rufaa kama NEC. Natambua inavyoumiza lakini mtafanya nini.
 
Kwan huyu askofu kapigiwa kura na Akina nani, maana anashutumiwa Sana, pengine walio mpigia kura ndio wahuni wabobezi,
AU nao kkkT wanaiba kura kama NEC,

Malasusa Sio muhuni pekee, kkkT Kuna wahuni wengi sana yan
Hakika
 
Tunaomba uzi wa mabadiriko mapya ya katiba mama ya KKKT.
 
Nionavyo mimi hamkufurahishwa na Dr.Malasusa kabisa. Jaribuni kuvumilia tu kule hawakati rufaa kama NEC. Natambua inavyoumiza lakini mtafanya nini.
Aliyeumia ni Benson Bagonza wa Karagwe, Stephen Munga wa Kaskazini Mashariki na Ambele Mwaipopo wa Ziwa Tanganyika.

Bagonza anaishi kuipinga serikali na chama tawala, anapinga Kanisa lake KKKT Tz na huenda anajipinga mwenyewe kwenye Dayosisi yake aliyojipa kuwa Askofu wa kudumu; maana Roho wa kupingapinga anamtumikisha ndani yake. Kuna rekodi yoyote ya Bagonza kuisifia serikali?

Munga roho wa kupingapinga alimsahaulisha asijipe Uaskofu wa kudumu na sasa yuko kwenye majuto ya kustaafu wakati asali ndiyo iko tayari. Munga tangu akiwa Mkwawa Sec akilala double-deck-bed 1 na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Capt. Makongoro Nyerere ambaye naye pia kama rafiki yake Munga ana Roho wa kupingapinga ambapo aliwahi kumpinga rais Nyerere (babake) na 2000 alibwaga manyanga CCM na kukimbilia NCCR-Mageuzi. Askofu Munga aliimarisha enzi yake na kutamani angeondoa herufi "a" kwenye jina lake Munga aweke herufi "u" lisomeke Mungu (Stephen Mungu). Halmashauri Kuu ya DKM ilimvua hadhi ya Uaskofu (baada ya mgomo) kwa hatia kadhaa zikiwemo:-

1. Kufuja milki/mali wakfu zilizo katika mfumo wa fedha ambazo zinatoka vyanzo vikuu vya sadaka na fadhila.

2. Siasa na uanaharakati.

3. Madeni ya SEKOMU (Sebastian Kolowa Memorial University) cha Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yanakiweka chuo katika hali ya kuparara.

Mwaipopo bendera fuata upepo unaoitwa "BagonzaMunga Wind" lakini bila kutengeneza jina kwanza kwenye tasnia za siasa na uanaharakati, mtaji unamkatikia mwanzo wa msimu wa mavuno. Hawezi kupapura wanasiasa na system ambao wana ngozi ngumu.

KKKT Tz kum-recycle Malasusa kama mkuu wake ni wazi kuwa enzi za huo utatu-usio-mtakatifu umekoma kama ilivyokoma enzi ya Askofu (Mst) Dr. Peter L. Mwamasika wa Dodoma (the firebrand wide-mouthed Bishop).

Malasusa ni mtoto wa mjini kingi-yake-hailiwagi kwenye mchezo wa chess.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo Kaisari Nero hayuko tayari kufanya kazi na Mitume Paulo na Petro. (Uwili-Mtakatifu lakini sumu kwa Nero)

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Maaskofu wa KKKT hamuendi mbinguni kwa kuweka KKKT kwenye milki ya CCM
KKKT inakuwaga kwenye chama cha siasa kutegemea Mkuu aliyeko madarakani.

Mfano, wakati Shoo yuko madarakani KKKT ilikuwa kwenye milki ya CHADEMA.

Case study:
Shoo alimshambulia RC Makonda hadharani kwenye ibada bila kujali itifaki kwa kuwa tu RC alikuwa kinyume na Mbowe wa CHADEMA ilhali RC ni CCM na Msukuma kama mteuzi wake.

Shoo huyo huyo juzi hajamshambulia Mwigulu aliyesababisha Makanisa kusuasua kwenye sadaka kwa kuweka tozo nyingi zinazopunguza vipato vya waumini na kuwaambia wasiotaka wahamie Burundi ambayo hii maana yake ni kwamba wafuasi wa nyumba wakfu za ibada wapungue idadi Tz wakaongezeke idadi kwenye nyumba wakfu za ibada za Burundi.

Nilijuwa juzi hii angemtoa nyongo Mwigulu kama alivyomkamua kamasi RC Makonda. Labda kwa kuwa Mwigulu hakumgusa Mbowe Mchaga.

Malasusa yeye awapo madarakani KKKT inakuwaga kwenye milki ya CCM.

KKKT hainaga permanent position kama Katoliki ilivyo neutral (Katoliki inaangalia tu... serikali, haiangalii chama, kwa sababu hata huko upinzani pia kuna wafuasi wa Katoliki wengi tu.

Katoliki ingeangalia chama badala ya serikali Dr. Slaa wa CHADEMA angeshinda urais 2010 kwa sababu Kikwete alikuwa Muislamu siyo Mkatoliki).

Katoliki walikuwa tayari Muislam Kikwete awe rais badala ya Dr. Slaa Padre mwenzao.

Wakati Nyerere anamkampenia Mkapa Askofu Munga alimuuliza Nyerere eti kwanini zamu hiyo isingekuwa ya Walutheri kutoa rais? Jibu alilopewa na Nyerere nali-reserve (si unajuwa majibu ya Nyerere kwa swali lililopishana na matamanio yake).

KKKT wanahitaji kupata darasa la Katoliki.

Something is wrong somehow somewhere in ELCT!

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…