Kizungumkuti cha mapenzi hii ni kali ya mwaka

SIPIYU30

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,224
2,000
Nimekaa zangu kwa ofisi, mara kaja office mate wangu, kama kawaida, baada ya kazi kunoga tunapiga story mbili tatu kuhusu maisha. Nikatoka zangu kwenda ATM mashine kuangalia kama salio limesoma maana mpaka jana lilikuwa bado. Nikakuta muamala wangu uko fresh, nikaja kumpa taarifa. Mara akapiga simu, kumwambia huyo mtu (on phone) kwamba niletee huo mzigo. Alipokata simu, few minutes kweli kaja mdada mrembo sana, mtulivu, anaongea kwa staha, duh kapendezaje? Mara office mate wangu kakabidhiwa simu kali, in exchange, akapewa 100,000/- nikabaki kukodoa mimacho tuu maana thamani ya simu na hela iliyotolewa havina uhusiano. Baada ya muda yule mrembo akaondoka. Tukabaki na story zetu. Ndipo akaanza kunisimulia kilichotokea.

Ni kwamba yule mrembo aliyekuja na simu alikuwa na mchumba wake na wakapanga kuoana. Huyo mwanaume kwao matawi ya juu hela si tatizo, na ana biashara zake kwenda nje ya nchi kama China, South Africa, Dubai etc. ni kama kutoka Kimara kwenda kariakoo. Wakafanya mipango yote na ikafika muda wa kupelekana kwa wazazi kujitambulisha. Wazazi wa mwanaume wakakataa, kumbe huyu mrembo alishawahi kugongana na wifi mtarajiwa na kupigana bifu za nguvu huko nyuma. Wifi mtarajiwa akawashawishi wazazi na wazazi wakakubaliana naye na hivyo kukataa ndoa hiyo kufungwa.

Kilichofuata, wazazi wakamtafutia mwanaume binti wa kuoa, jamaa hakukataa na wala hakukubaliana nao, ila akawa hana msimamo akajikuta akifunga ndoa na huyo chaguo la wazazi, lakini hakuwahi kukutana na huyo binti wala kushiriki vikao vyovyote. Baada ya ndoa kufungwa, jamaa akamtamkia live mke wake kuwa wewe si mke wangu ila mke wa wazazi wangu. Akawa anaendeleza mahusiano na huyu mchumba wake wa zamani.

Huyu mchumba amepangishiwa nyumba nzima na mahitaji yote, yaani kila kitu anachotaka anapewa. Jamaa anakwenda kwake, anakaa mpaka usiku saa saba usiku ndo anarudi kwake, na akiulizwa anajibu hovyo. So far, huyu mchumba wa zamani ameshanunuliwa kiwanja tena kikubwa, kikiwa na hati na ujenzi unaanza wakati wowote. Hivi karibuni mshikaji ametoka nje na zawadi mbalimbali zenye kujaza sanduku na mojawapo ni simu Samsung ambayo kibongo bongo siyo chini ya laki 7 kwenda juu (ni makadirio tuu). Ndo akamwambia hataki kumwona na hiyo simu aliyokuwa nayo maana anataka kumwona na hiyo mpya. Ndo maana mrembo kaja kuiuza kwa office mate wangu kwa bei ya kutupa, ni kama kampa zawadi.

Huyu mchumba sasa amepata mchumba mwingine ambaye anataka amuoe. Sasa kizungumkuti ni hiki. Mke halali wa ndoa wa jamaa anajua hapendwi, lakini hataki kuachana na mwanaume japo anatukanwa ameganda hapo. Mchumba wa zamani ana mapenzi ya dhati kwa jamaa, lakini haolewi na hataki kumwacha. Kwa sasa ni kama hajielewi, kunyoa au kusuka. akiolewa mirija inakata, asipoolewa atakaa hivyo mpaka lini bila mume, japo anapata kila kitu. kwa haraka naona wanaume zaidi ya watatu wakishea mapenzi na wanawake zaidi ya watatu.

Hivi katika mazingira haya, tujiweke ktk nafasi ya wahusika na tujadili. Inauma lakini ndo hivyo imeshatokea. Mimi binafsi namlaumu sana mwanaume kwa kutokuwa na msimamo.
 

PLL

JF-Expert Member
Jan 22, 2013
882
195
Hahaha raha!ila yamkute mwenzio yasikukute wew!kama vp asiolewe maana huyo atakaemuoa atapata shda sn!
 

venine

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
1,379
2,000
Kila mara tunawaambia humu wanaume lazima muwe na misimamo, wazaz wanashauri ila decision za maisha yenu ni zenu, km alimuoa asiyempenda ndio hivyo ataishi unhappy life mpaka kifo kiwatenganishe.

Kutofata advice ya wazazi doesnt mean u disrespect them.
 
Top Bottom