Kizungumkuti cha gesi

Kizungumkuti cha gesi

Hon.MP

Senior Member
Joined
Jul 15, 2012
Posts
153
Reaction score
86
attachment.php

Wajuvi wa kupiga ramli hasa Mwita Maranya yule mkulima wa mboga na kipenzi chake kiongozi wa Masalia (mzee wa dawa za panya aliyeaga kwao) watujuze ni nini hasa KIZUNGUMKUTI CHA GESI.
 

Attachments

  • chadema.jpg
    chadema.jpg
    64 KB · Views: 473
Je,Viongozi wetu wanaujasiri wa kuelezea kilichopo nyuma ya pazia la Uchimbaji gesi Mtwara?
 
Wajuvi wa kupiga ramli hasa Mwita Maranya yule mkulima wa mboga na kipenzi chake kiongozi wa Masalia (mzee wa dawa za panya aliyeaga kwao) watujuze ni nini hasa KIZUNGUMKUTI CHA GESI.

Kizungumkuti hakuna kwa sababu

1. Ukweli wa mradi haujulikani zaidi ya kuwa Rais Dhaifu amewapa wa China mradi na rasilimali hiyo kumwokoa mwanae asinyongwe.

2. Manufaa kwa wana kusini hayajulikani kwa sababu yakijulikana mafisadi watajulikana na kuadhirika.

3. Mizania inasemaje tumekopa china, tutarudishaje mkopo kwa faida zipi za kitaifa.

4. Ilani ya CCM iliuzwa kwenye uchaguzi au iligeuzwa? Kwa nini sasa kuna kizungumkuti.

Serikali ya mfukoni mwa JK dhaifu haina majibu kwa sababu ilitegemea kuwa watu ni watazamaji tu mambumbumbu hawana haki.

HAKUNA KIZUNGUMKUTI KUNA MCHEZO UNAITWA "UKUTI WA MNAZI"
 
Ni ukweli usiopingika kuwa tuna Wabunge wenzetu ambao ni Wanasiasa uchwara tulionao bungeni ambao nawaita ma-agent wa mafisadi waliotaka kusambaza mafuta feki na pia wale wenzao wanofisadi TANESCO kupitia mapato ya majenereta yao. Ni hawa ambao wanaoshangilia tuwapo gizani maana hiyo ndiyo mitaji yao. Wanaonekana kuhangaika sana kutokana na misimamo na uadilifu wa Watendaji wa sasa wa Wizara ya Nishati na Madini. Mbinu zozote wanazopanga za kuanzisha vurumai ndani ya Wizara hiyo zimeshindwa kwa jina la umoja!
Serikali itable hiyo sera ya gesi ijadiliwe na wadau wote husika; Wizara ikamilishe mpango wa upatikanaji na usambazaji wa gesi kwa ufanisi- Wananchi wa Mtwara na Watanzania wote kwa ujumla tunufaike.
Ili kuisimamia Serikali vyema na kusafisha uozo nje; tunatakiwa kuanza ndani ya Bunge kwa kuwachomoa hawa ma-agent wa mafisadi Bungeni. Tutawakaba kooni muendelee kuwa masalia!!!
 
Kizungumkuti ni KUUONA MKATABA WA MRADI HUU MAANA NI SIRI.
"Ni siri kwa sababu , mikataba hii ikiwekwa wazi unakuwa unahatarisha maslahi ya makampuni yanayohusika kwenye hii mikataba katika masuala ya ushindani na makampuni mengine...kwani washindani wa makampuni haya watajua nguvu za mshindani wao. Na sisi hatutaki kuhatarisha maslahi ya wawekezaji wetu wenye tija kwa taifa..." Mtawalaalisikika akitetea hoja ya kuhakikisha mikataba inabiki kuwa siri.
 
Back
Top Bottom