Kizimbani kwa kukutwa na noti bandia

Kizimbani kwa kukutwa na noti bandia

Hearten

Member
Joined
May 17, 2016
Posts
46
Reaction score
54
EC-p15GXYAA9sHO.jpg

Mkazi wa Magomeni Mapipa Mariam Zuberi (21), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kukutwa na noti 20 za bandia.

Akisomewa hati ya shtaka mbele ya Hakimu Lilian Silayo na mwendesha Mashtaka wa Serikali Ester Charles amedai mnamo Juni 27, 2019 eneo la Magomeni Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam bila kuwa na idhini ya mamlaka husika, alikutwa na noti 20 za bandia za sh 10,000 zenye thamani ya Sh 200,000.

Noti hizo zina namba za usajili GF4658564 noti 5, GF4658572 noti 4, GF4658567 noti 3, GF4658561 noti 2, GF4658562 noti 2, GF4658563 noti 1 na BK8169395 noti 1 huku akifahamu kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo mbele ya mahakama, huku upande wa Jamuhuri ukisema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kesi kusikilizwa tena.

Hakimu Silayo amesema fungu la dhamana liko wazi kwa masharti kwa kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi katika taasisi zinazo tambulika kisheria na nakala ya vitambulisho vinavyotambulika na serikali ambao watasaini bondi ya Sh 500,000 kwa kila mdhamini.

Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuachiwa mpaka kesi yake itakaposikilizwa tena Septemba 26 Mwaka huu.

-Mtanzania-
 
Ila watu niwataalam kubutua, mimi hata org na fek sijui kutofautisha.
zinauzwa unatoa 40000 ya ukweli unapewa noti za 10,000 za LAKI

unatoa 50,000 ya ukweli unapewa noti za 5000 za LAKI (noti za 5000 ni bei kdg)

unatoa 60,000 ya ukweli unapewa noti za 2000 za LAKI (noti za 2000 ndio bei kuliko zote)

unatoa 40,000 ya ukweli unapewa noti za 1000 za LAKI

UPDATE

coin za 500 zinakuja...nshaishuhudia moja ya mAJARIBIO mama weeeee zikija kweli itakua ni vilio na kusaga meno...

kuigundua coin ya jero geuza upande wa NYATI yule nyati kakosewa sana amekaa kama kituko,ila ukiangalia upande huu wa BABA WA TAIFA kitu ng'adaaaaaa.
 
Njia rahisi ya kugundua NOTI og na Feki ambayo watu hawajaijua na nyepesi ukitoa kukunja kunja noti,au kuiangalia juu kwenye mwanga kumtafuta twiga na ule mstari wa kung'aa.

Njia nyepesi kwangu ni KUNUSA NOTI HUSIKA...nusa Hela unayopokea Harufu ya NOTI OG sidhani kama kuna asiejua harufu ya NOTI ORIGINAL...harufu ya NOTI FEKI/BANDIA aseee sio ya kawaida..kwa ataezifumania ajaribu kuzinusa atagundua utofauti.

Mungu hakukosea kutupa PUA
 
Hakuna kesi hapo.
Kama wamekubali wadhamini wa kuweka bondi ya laki 5 tu hawezi kushindwa.
Kimbembe ukamatwe na meno ya tembo au ngozi ya twiga ndio utaijua rangi ya Jamhuri.
 
zinauzwa unatoa 40000 ya ukweli unapewa noti za 10,000 za LAKI

unatoa 50,000 ya ukweli unapewa noti za 5000 za LAKI (noti za 5000 ni bei kdg)

unatoa 60,000 ya ukweli unapewa noti za 2000 za LAKI (noti za 2000 ndio bei kuliko zote)

unatoa 40,000 ya ukweli unapewa noti za 1000 za LAKI

UPDATE

coin za 500 zinakuja...nshaishuhudia moja ya mAJARIBIO mama weeeee zikija kweli itakua ni vilio na kusaga meno...

kuigundua coin ya jero geuza upande wa NYATI yule nyati kakosewa sana amekaa kama kituko,ila ukiangalia upande huu wa BABA WA TAIFA kitu ng'adaaaaaa.
broo shkamoo.....unajua mpaka unakera..najazia...elfu mbili zikiwa tano ambapo jumla ni elfu kumi(10000),ina thamani kuliko 10000 moja..kwasababu elfu mbili ni ngumu kugundulika..inayofuatia kwa thamani ni 5000 na yw mwisho ni 10000
 
ni kweli 2000 zinatembea sana kugundulika mpk ukute mtu alishawahi kutana nayo..

watu wengi wamekariri noti feki ni za 10,000 tu hata zinazodakwa ni burungutu za 10,000 ila sio buku au buku 5.

ukiona ivyo ujue nshalizwa sana so ikabidi hadi nigharamike kupata elimu ya UTAMBUZI otherwise sisi tunaocheza na PESA daily tusio na mashine tunahesabu kwa mikono TUNGEKUA TUNALIZWA MNO MNO.
 
zinauzwa unatoa 40000 ya ukweli unapewa noti za 10,000 za LAKI

unatoa 50,000 ya ukweli unapewa noti za 5000 za LAKI (noti za 5000 ni bei kdg)

unatoa 60,000 ya ukweli unapewa noti za 2000 za LAKI (noti za 2000 ndio bei kuliko zote)

unatoa 40,000 ya ukweli unapewa noti za 1000 za LAKI

UPDATE

coin za 500 zinakuja...nshaishuhudia moja ya mAJARIBIO mama weeeee zikija kweli itakua ni vilio na kusaga meno...

kuigundua coin ya jero geuza upande wa NYATI yule nyati kakosewa sana amekaa kama kituko,ila ukiangalia upande huu wa BABA WA TAIFA kitu ng'adaaaaaa.
za kutoka Kenya kugundua ni kazi sana
 
[emoji119]Biashara nzuri sanaa hii.
 
ni kweli 2000 zinatembea sana kugundulika mpk ukute mtu alishawahi kutana nayo..

watu wengi wamekariri noti feki ni za 10,000 tu hata zinazodakwa ni burungutu za 10,000 ila sio buku au buku 5.

ukiona ivyo ujue nshalizwa sana so ikabidi hadi nigharamike kupata elimu ya UTAMBUZI otherwise sisi tunaocheza na PESA daily tusio na mashine tunahesabu kwa mikono TUNGEKUA TUNALIZWA MNO MNO.
Hivi kati ya Noti feki na Cheti feki ni kipi kina kazi ngumu ya kugundulika?
 
ATM huwa hawaweki fedha bandia? Maana ATM za NMB utakuta hela chafu na hazieleweki mpaka unaogopa.
 
Hahah UNADABULIWA sio [emoji23][emoji23][emoji23]
nzuri kweli chief..sema ukiwa unalala usiku ndoto zako zote utakua unaota MAISHA YA JELA yatakavyokua siku ukidakwa.

Hutokaa uote hata siku 1 unaendesha BMW au FERARI ndoto zote zitakua ni za jela jela jela...na zikizidi hizo ndoto huchukui ROUND unadabuliwa.
 
Back
Top Bottom