MJ, sikuhizi wakazi wote wa Mbezi baada ya Lugalo wanajiita wa Mbezi Beach! wakimaanisha Dar kuna Mbezi mbili ile ya Kimara na hii ya Beach , jee umeshasikia Tegeta Beach? nako ni Mbezi Beach.<br />
<br />
Zamani kuna watu wakisoma Mbuyuni huku wakijiita walisoma O'bay!. Kuna watu wanaoishi Buguruni huku wakisoma Tambaza wanapanda mabasi ya Posta then ya Mwenge na kushukia Palm Beach na kujiita watoto wa Upanga!. Ndiyo haya sasa ya Kunduchi Salasala kuitwa Mbezi Beach ili kuhalalisha kaeneo ka high density kuizwa kwa milioni 28!.