Gazillionaire
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 235
- 59
- Thread starter
- #21
Mkuu Erigue heshima yako
Mimi nafikiri kwa mazingira uliyo kutana nayo katika hii kesi yako uliamua kufanya conclusion kuwa jamaa ni tapeli kwa hilo sikulaumu,lakini kuna kila ushahidi wa kwamba huyu jamaa sio tapeli sababu amekuwepo hapa jukwaani kwa kutumia ID hii na namba ni hiyohiyo hajawahi badilisha.
Mimi ni mfuatiliaji sana wa matangazo ya viwanja na mashamba na huyu Dalali nimeshaona matangazo yake mengi sana kwa ID hii na anatambulika sana hapa jukwaani.
Kubwa kuliko yote nimesha fanya naye biashara na nilianza kumjua huko zoom baada ya kuona tangazo lake la shamba kigamboni.
Baada ya kusoma hii conversation yenu naona tatizo lipo kwa dalali sababu hakufanya verification ya mmiliki wa eneo,Yeye kama Dalali huwa anatafutwa na wamiliki ili atafute mteja hivyo hata yeye alikupeleka kwa kudhani ni mmiliki halali kumbe sio.Katika hili mkuu Gazillionaire inabidi ujifunze
Ulicho kifanya ni kibaya sana mkuu erique,ulitakiwa kumface mwenyewe na ikiwezekana kumshitaki kwa moderators sababu ID yake unaijua na mlionana face to face.Una muharibia mwenzio kazi yake kwa jambo ambalo kama ungechukua muda kidogo kulitafiti ungejua ukweli.Shutuma zako ni nzito sana aisee
Binafsi sina shaka na huyu Dalali na tumesha fanya biashara hana shida
Nashukuru sana Mkuu, angalau wewe umemwelewesha, imenipa relief kuwa hata ushahidi humu jukwaani upo juu ya sincerity yangu kikazi. Nakiri kuwa nilifanya kosa kutoverify thoroughly umiliki halali wa eneo, lakini pale nilipopata taarifa, I took action kwa kuwanotify wateja wote waliokuwa wana interest na wengine nikawaaambia pameuzwa ili wasisumbuke kupiga tena. Na kuna mmoja mpaka aling`ang`ania kuendelea na manunuzi tukafikia kutaka kugombana akidhani nimepeleka mtu mwingine. Milioni 2 ni hela nyingi sana, lakini siwezi nikarisk kazi yangu na uaminifu walionipatia watu kwa hela hiyo. Siwezi kuhama mjini kwa milioni 2.