Nilitaka kukuibia wapi? Mimi si ndie niliekuonya? Nikuibie kwa faida gani hasa? Acha biashara ya kuchafuana. Kila mtu alie humu anaifahamu namba yangu na ID yangu na wengi nimefanya nao biashara na watakuja kusema hapa, leo wewe umeibuka na kashfa ya kitoto kuwa nilitaka kukuibia, eleza ni kwa vipi hukuibiwa kama sikukuonya Mimi. Toa ushahidi la sivyo nakushtaki kwa sababu nakufahamu na uzitaje hizo IDs nyingine. Niko serious, hili swala litafika mbali
Mzee acha usanii bwana,mimi siwezi kujibishana na wewe hapa kwasababu haitanipa faida, isitoshe wewe unajua ulichotaka kunifanyia. Mimi nachohitaji ni kuwafahamisha wengine ili wawe makini. Wadau mimi ngoja niweke wazi hapa ilivyokuwa. Huyu bwana nilipata kuliona tangazo lake la kuuza mashamba huko Mwasonga Kigamboni, nikaona niwasiliane nae na tukakubaliana kukutana ili niende kuona hilo shamba. Tulipokutana na wkati tupo njiani kuelekea kwenye hilo eneo akawa anawasilaiana kwa simu na mtu, amabaye yeye alikuwa akimuita ndio mmiriki.Tulipofika tukakutana na huyo kijana, na nikaonyeshwa hilo eneo, na eneo lote lilikuwa na jumla ya ekari 25. Bei aliniambia ni milion 1.2 kwa ekari moja, na tukakubaliana nichukue ekari 2. Nikazungushwa eneo lote na kuonyeshwa mipaka, na hatimaye nikachagua eneo ninalolihitaji.
Mimi sikuwa na hela kwa wakti huo, so tulikubaliiana ningerudi kulipa hela weekend iliofuata. Cha kushangaza yule aliekuwa anajiita mmliki alikuwa analia njaa sana, kwamba niwape hela kidogo ili asije kuliuza. Nakumbuka nilimwambia ww kama ndio mwenye shamba inakuwaje unakuwa na maisha magumu na usikate ukauza kidogo, maana eka 25 ni nyingi na kama hufanyi kitu hapo ni bora ukapunguza kwa kuuza. Mwishowe nikaona isiwe taabu, nikampatia elf 50, na kisha huyu bwana Gazziliionaire nikampatia elf 20.
Wiki iliofuata, bila hawa mabwana kujua mm nilirudi lile eneo, na kuwasiliana na majirani, majirani walianza kunipa pole, kwamba hili eneo linamilikiwa na watu tofauti tofauti, na kama nitakuwa nimeshalipa hela basi nitakuwa nimeibiwa. Nikaona isiwetaabu nikaenda kwenye serikali za kijiji, nikamchukua mwenyekiti na mtendaji mpaka eneo lenyewe, na ndio hapo sasa wakanihakikishia kwamba huyu bwana ni TAPELI, na amekuwa akileta watu wengi eneo hilo, na wamefanikiwa kutapeli watu kadhaa kwa eneo hilo. Na wakasema kihalali, hilo eneo linamilikiwa na MUHINDI fulani, ingawa kuna wengine wameshauziwa kwa utapeli pia. Bila huyu bwana kujua kama nimeshashitukia mchezo yeye aliendelea kunisumbua na kunikumbusha niende kulipa. Huyu bwana anabadilisha badilisha ID na pia ni dalali wa NYUMBA, na pia anapatikana kwenye mitandao mingine kama zoomtanzania.
Nachoweza kuwashauri watu humu, kama unaamua kununua eneo lolote huko, hakikisha unaenda kwa serikali za Mtaa, na pia ujihakikishie kwamba huyo anaejiita mtendaji au mwenyekiti ndie mwenyewe kweli, maana unaweza kuingizwa ofisi ya mtendaji kumbe huyo aliyepo sie mwenyewe, ila ni tapeli pia wanaoshirikiana. Ni vizuri ukauliza majirani wakakufahamisha mtendaji ni nani na mwenyekiti ni yupi. Kuweni Makini