Kiwango cha silaha za nyuklia chapungua duniani

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Ripoti mpya iliyochapishwa leo imesema kiwango cha silaha za nyuklia duniani kimepungua katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita lakini mataifa ulimwenguni yanatengeneza silaha za kisasa zaidi.

Kulingana na makadirio ya Kituo cha kimataifa cha utafiti wa amani cha Stockholm (SIPRI) mwanzoni mwa mwaka 2019 mataifa tisa ulimweguni yalikuwa na shehena ya silaha 13,865 za nyuklia.

Idadi hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na mataifa ya Marekani, Urusi, uingereza, ufaransa, China, india, Pakistan, Israel na Korea kaskazini ni pungufu ya silaha 800 za nyuklia ikilinganishwa na mwaka 2018.

Hata hivyo SIPRI imesema mataifa yenye silaha za nyuklia yanaboresha shehena zao silaha huku China, india na Pakistan zinaongezeka kiwango cha sialaha zake za nyuklia.

SIPRI imesema mafanikio hayo yanatokana na mataifa ya Urusi na Marekani kutimiza wajibu wake kwenye mkataba wa mwaka 2010 unaoweka kikomo cha umiliki wa silaha za nyuklia.
 
Sawa. Ingawa inaonekana kuna kupungua huko kunakosemwa ni mafanikio makubwa lakini hivi sasa uundaji wa hizi silaha unahusisha Teknolojia ya kisasa zaidi kadri siku zinavyoendelea. Kinachopungua ni Quantity tu lakini hizo chache zinazozalishwa ni More Advanced na zina uwezo mkubwa zaidi.

Ukitizama tu hasa katika Delivery Systems zake zinavyozidi kuboreshwa zaidi katika; Accuracy, Capacity, Speed, n.k. utaona How Modified They Are. Na Delivery Systems ndiyo moja ya Factors kuu ambazo zinaipa nguvu silaha yako kushambulia kwa ufanisi zaidi.

Siku hizi tayari kuna Missiles zenye Multiple Targets. Pia kuna zenye uwezo wa kuhama uelekeo na kuzipoteza Anti-Ballistic Missile Systems na siku si nyingi kutakuwa na vitu kama Ballistic Missiles zenye Nuclear Reactor ambazo zinaweza kuzunguka angani kama Satellites kwa muda mrefu zikisubiri Directions kutoka chini. Teknolojia inaongezeka zaidi.
 
najiuliza tu kwamba hizo zilizopungua zimekwenda wapi hali ya kuwa hakuna mapigano ya kihivyo yaliyohusisha matumizi ya hizo silaha za nyuklia
 
Kuna sehemu maalumu za kuziteketeza. Mfano kwenye mkataba wa kupunguza silaha za Nyuklia Kati ya Marekani na Urusi,wakati wa kuteketeza kama Marekani anateketeza idadi na aina fulani lazima wawakilishi/Wataalamu wa Urusi lazima wawepo washuhudie.
 
kama ni kweli sawa ila bado nina kigugumizi kwenye kuamini hili[emoji23]
 
In Real Sense, ni kama tu wanaziharibu Delivery Systems zake ambazo ndizo hutumika kubebea hizo silaha na si kuteketeza silaha yenyewe. Mfano wa hizo Delivery Systems ndiyo hayo makombora ya Nyuklia. Ndiyo maana hata hii mikataba mbalimbali ya kupunguza silaha za Nyuklia unakuta inazuia aina fulani tu ya makombora na si aina nyingine.
 
hapa labda lakini kusema wanaharibu kabisa nyuklia mmh aisee[emoji2089]
 
Sawa. Ingawa inaonekana kuna kupungua huko kunakosemwa ni mafanikio makubwa lakini hivi sasa uundaji wa hizi silaha unahusisha Teknolojia ya kisasa zaidi kadri siku zinavyoendelea. Kinachopungua ni Quantity tu lakini hizo chache zinazozalishwa ni More Advanced na zina uwezo mkubwa zaidi.

Ukitizama tu hasa katika Delivery Systems zake zinavyozidi kuboreshwa zaidi katika; Accuracy, Capacity, Speed, n.k. utaona How Modified They Are. Na Delivery Systems ndiyo moja ya Factors kuu ambazo zinaipa nguvu silaha yako kushambulia kwa ufanisi zaidi.

Siku hizi tayari kuna Missiles zenye Multiple Targets. Pia kuna zenye uwezo wa kuhama uelekeo na kuzipoteza Anti-Ballistic Missile Systems na siku si nyingi kutakuwa na vitu kama Ballistic Missiles zenye Nuclear Reactor ambazo zinaweza kuzunguka angani kama Satellites kwa muda mrefu sikisubiri Directions kutoka chini. Teknolojia inaongezeka zaidi.
dangerous
 
Back
Top Bottom