Hutomuuzia mtu wa nje nyama uliyosindika hapa nchini, unaweza fatilia vigezo vya kuwa supplier wa foodstuffs kwa nchi za nje. Huwezi fuga nguruwe ukawauzia China hivihivi, nguruwe wao wanatoa US na Germany kwa sana. Mpaka usaini nao mkataba, na wakague ubora wako.
Vietnam wanauza kambale kwa US, toka hapa beba tani za kambale peleka US uone kama utaziuza.
Ukiona wabongo wanapeleka ng'ombe Shelisheli uko usidhani hawawezi kufanya slaughtering na kuuza nyama. Tatizo soko unalo?
Unajua mkataba ya nchi kama EU ya kuuziana bidhaa. Nchi kama Netherlands inauza dairy products kwa UK, wewe upeleke pua yako kama nani. Wanalindana masoko yao, ukitaka kuwauzia lazima kuwe na mikataba. Toka hapa acha kuwauzia Kenya maua uyapeleke mwenyewe uone kama utayauza. Wazungu wanafanya biashara kama dalali na mwenye nyumba.