Guyz, EATV hamna kipindi kama hicho. Kipindi ninachofahamu mimi kinaitwa Friday Night Live na siyo Saturday Night Live. Sometimes tusiwe tunatetea au kuunga mkono ujinga. Kweli mtu uingie studio umevaa malapa, pensi na umelewa halafu mtangazaji akuchekee tu! Tusiwe tunadharau ofisi za watu eti kisa we msanii. Ustaarabu ni kila kitu. Angekuwa amevaa vizuri na kichwani yuko vizuri angerudishwa? kwani ni mara ngapi amekuwa akifanya interviews kwenye kipindi hicho hicho akiwa yuko sawa bila kurudishwa?
NB: Zaidi ya kumjua Sam kupitia vipindi anavyoendesha, sina uhusiano wowote naye. Kama vipi na yeye ajitokeze aeleze yake.