MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Inaelezwa kua kuelekea uchaguzi wa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mwishoni mwa juma lijalo kuna misuguano mingi ya ndani kwa ndani inayokikumba chama hicho cha siasa kukibwa na kikongwe nchini, misuguono hiyo inaashiria kuwepo kwa kambi mbili zinazotofautiana kwa kiasi kikubwa kuhusu kufanyika kwa uchaguzi huo unaovuta hisia za makada wengi ndani ya chama hicho.
Kufuatia misuguano hiyo pia kunaelezwa ni kutokana uwepo wa wafuasi wa aliyekua mgombea urais kupitia vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa.Kwa minong'ono ya baadhi ya makada ndani ya chama ni kwamba wanachama hao hawataki kuona kabisa kua mkuu wa nchi ambaye anatarajiwa kupewa kijiti hicho na mwenyekiti anayemaliza muda wake Rais mstaafu Mh Jakaya kikwete, sababu kubwa ni hofu iliyowatanda kuhusu maisha yao ndani ya chama ikiwa huyu Mkuu mtarajiwa na pengine ndiye atakua mwenyekiti wa chama taifa.Hii inasababishwa na kinachoitwa usaliti waliouonesha wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka Jana 2015 kutokukubaliana na kukatwa kwa jina la Edward Lowassa hadharani.
Kuna kundi ambalo linapenda kuona kua Mwenyekiti wa sasa anakua Rais wa sasa ili kuendeleza kasi yake ya kuyatumbua majipu na kutoyaonea haya makundi yanayopelekea chama kugawanyika. Hili ni kundi ambalo linadaiwa kuamini kwamba endapo Mh Rais akiwa mwemyekiti wa chama bado hatoweza kuyalea baadhi ya majipu yaliyoota mizizi ndani ya chama siku nyingi.
Kuna mijada iliyoipbuka mitandaoni ikionesha baadhi ya makundi ya makada wa chama cha mapinduzi wakiwalaumu wenzao kufanya hujuma kuzuia uchaguzi usifanyike kama ilivyojarajiwa kwa maslahi yao binafsi. Hii imesababisha mabishano makali baina ya kundi na kundi kuonesha kua hali si shwari kuelekea siku ya uchaguzi huo.
Baadhi ya makada watiifu wa CCM wamesikika wakidai kua kuna baadhi ya viongozi waandamizi wa sasa ndani ya chama wanatumia muda mwingi na rasirimali za chama kuzunguka nchi nzima kushawishi wajumbe sehemu mbali mbali kuwepo na mgombea zaidi ya mmoja kama katiba ya chama inavyosema ili wachague watakaomtaka.
Hivyo hili kundi linalodaiwa kua lilikua linamtii ndugu Edward Lowassa bado haliaminiwi ndani ya chama, bado lina msimamo tofauti kuhusu ujio wa mwenyekiti mpya ili kuepuka kikombe cha kutumbuliwa.