Kiukweli hakunaga mtu bize kama yule ambaye anaona huna thamani

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,407
19,071
Kuna watu vipofu nami naleta msaada kuwatoa hicho kilemba kinacho waziba macho. Binafsi nina msemo, ukinichukulia kama kituko basi nakuacha kama utani

Kiukweli hakunaga mtu bize kama yule ambaye anaona huna thamani, iwapo ungekuwa na thamani kwake nakwambia atafanya lolote muonane hata kwa nusu saa.

Hata mimi kabla ya kumpata huyu mke wangu asikwambie mtu nilikuwa bize sana tu lakini nikisikia sauti laini ya huyu mtoto akili ilikuwa inahama kushoto kabisa, nilidiriki hata kusingizia nlienda dukani kununua dawa ilimradi tu nione tavasamu lake, nimkumbate natupeane salamu macho kwa macho.

Na nyie mnaolalamikaga mtu yupo bize naombeni msimfanye mtu awe kipaumbele wakati yeye hukufanya kama mbadala, na sana sana atakuhitaji tu pale inapobidi labda akikosa kabisa kampani anayoipenda.

Mtu gawezi kuwa busy siku nzima, mtu atahangaika sana kuwepo anapopapenda, ndio maana hata hapa kazini tunaweza kutoka saa 12 lakini watu hufika kwao saa nne wakisingizia walikuwa busy kumbe walikuwa bize sehem wanazozipenda kwa watu wanaowapenda.

Haiingii akilini mtu hata kukutumia meseji "mchana mwema" hawezi, ubize wa namna gani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom