Kiufupi ni kama bodaboda hazitakiwi ila akufukuzae hakuambii toka

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,551
22,097
Kila nchi ina sheria na utaratibu unaotakiwa kufuatwa;

Watu wanapo nunua bidha huzingatia sheria za nchi zinasemaje; Sasa naomba kuzungumza kuhusu Hii bidhaa PIKIPIKI maarufu kama BODA BODA,

Tangu soko la boda boda lishamili kumekuwepo na figisu figisu nyingi sana za jeshi la police kupambana na BODA BODA, yaani hadi mefikia hatua sasa kwa BODA BODA kuishi kwa wasiwasi kama wauza Gongo. Kwakuwa;

1. Waliomba kiila pikipiki iweke namba nyeupe MC ..watu wakatii wakaweka ila bado ikawa haitoshi.

2. Wakataka kiila boda boda anayetaka kuja mjini akate kibali maalum watu wakatii ila haitoshi.

3. Wakata kiila bodaboda awe na leseni, watu wakatii ila haitoshi

4. Wakasema kiila boda boda aweke kiegemeo nyuma watu wakatii, ila haikutosha

5. Wakasema kiila bodaboda ajisajili kijiwe chake kama tax, watu wakatii ila haikutosha

6. Wakasema kiila boda boda awe na Helement mbili, watu wametii ila bado haitoshi.

Pamoja na hayo yooote bado nimeshuhudia pikipiki zinaendelea kukusanywa mafungu mafungu ila nayo bado haitoshi, Leo nimepita police eneo la MTONGANI wamejipanga barabarani wanawa lamba bakora maboda boda na wengine kwahofu kukimbia hadi wanaingia mtaroni, SASA HIZI BODA BODA KAMA HAZITAKIWI SI LITOLEWE TAMKO TU HAZITAKIWI KUWEPO NCHINI WATU WAJUE MOJA WAKALIME?. Hawa nao ni binadamu serikali inatakiwa kuwafikilia namna ya kuwahudumia, Vinginevyo, watu waambiwe vigezo vyote kwa pamoja ili watu wavitekeleze mara moja. Haya mambo yanavyo endelea ni sawa na AKUFUKUZAE HAKWAMBII TOKA.

“SITETEI UHALIFU AU UVUNJAJI WA SHERIA, LAKINI KAMA KUNA SHERIA ZIFUATWE NA SI KUWACHAPA BAKORA”
 
Hili swala kwa kweli linaumiza na kusikitisha sana kwa sasa,sasa hivi wameamua kuwafuata mpaka vichochoroni wanapopaki wanakamatwa na kupelekwa central then wanatozwa 120,000/= kwa kila boda boda. Ni heri Serikali kupitia Polisi itoe tamko kuwa boda boda haziruhusiwi popote pale pia wapige marufuku importation yake.
 
Waziri mkuu wa India anasema watajenga viwanda vya boda boda na bajaji. Kwa hali inayoendelea ya kamatakamata naanza Kuwa na mashaka ya soko la hizo boda boda. Hii nchi ina maswali magumu mengi sana... ambayo watawala wanatoa majibu mepesi
 
Kwa hiyo hayo madereva wa bodaboda mby wameamua kuchangia ujenzi WA wodi ya wao ili wakivunjika wapate pa kulala
 
bodaboda zinatakiwa ziwe regulated sana yaani ni majanga tupu, cheki mfano hii hapa

Mkuu Chinchilla Regulation/sheria zipo ila wasimamizi hawazitumi wala hawana habari nazo ni mzuka kwa kwenda mbele.
Kama ningepata msaada wa mtu anaejua sheria nakusudia kuishtaki serikali ya jiji..... Haiwezekani kibali cha kuendesha pikipiki mjini ni kikubwa 50 zaidi kuliko premium insurance huo ni wizi....
1.Mkuu Wajenzi sheria zipo nenda kwa wanasheria watakusaidia tatizo lako tafadhali.
2.Watumiaji waelimishwe kuzifuata sheria tatizo litapungua kama siyo kwisha.
 
Mkuu Chinchilla Regulation/sheria zipo ila wasimamizi hawazitumi wala hawana habari nazo ni mzuka kwa kwenda mbele.

1.Mkuu Wajenzi sheria zipo nenda kwa wanasheria watakusaidia tatizo lako tafadhali.
2.Watumiaji waelimishwe kuzifuata sheria tatizo litapungua kama siyo kwisha.
Yeah sure ila hii ni some kind of a movement ambayo nadhani wadau wana mchango mkubwa...... Hamna kituo chochote cha wanasheria kinachodeal na haki za kiraia?? Rip Mzee mtikila
 
Mbona juzi yule Muhindi wa India ni kama nilimsikia wataleta kiwanda cha Ku unga Pikipiki hapa na akashangiliwa sana?
Au tukiziunga tunaenda kuziuza tena India?
****
KIFIKRA NI KWAMBA BADO TUPO NYUMA SANA,
-->>KWANINI TUSINGELIOMBA WAJENGE KIWANDA CHA SUKARI?
-->>KIWANDA CHA KUTENGENEZA VITAMBAA VYA NGUO ZA KISASA?,WASIJE TUVALISHA JEREMANI /
--->>n.k/ ....
 
Back
Top Bottom