Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,118
- 1,565
Mhu 6:7 SUV
[7] Kazi yote ya binadamu ni kwa kinywa chake, Walakini hata hivyo nafsi yake hashibi.
Wakati mwingine tunafanya kazi kwa bidii sana kuhakikisha tunapata mahitaji yote ya kimwili, wapo watu wanafanikiwa sana katika hili.
Wapo watu wanahakikisha wanapata elimu bora, watoto wao wanasoma shule nzuri na vyuo vizuri, wapo wanafanikiwa sana kufika viwango hivyo.
Wapo watu wanafanikiwa kufanya kazi kwenye masharika makubwa na yenye mishahara mikubwa, kwao suala ya mahitaji madogo madogo ya kimwili inakuwa sio shida tena.
Wapo watu hawana shida juu ya gharama za matibabu, wana uhakika wa kutibiwa mahali popote pale, maana wanazo bima kubwa na pesa za kutosha kuhakikisha wanapata matibabu bora.
Maisha haya ya kimwili wapo watu wamefanikiwa sana kwenye maeneo mengi, wapo watu wamevuka viwango vya kuwaza chakula, maana yake kipo cha kutosha, hata wasipofanya kazi miaka 20 mbele wanaweza kula na kunywa.
Andiko hili la biblia linatuonyesha wazi kuwa pamoja na watu kufanya kazi kwa bidii kujipatia kipato na mahitaji mengine ya kimwili, bado kuna kiu ya ndani ya kila mtu haiwezi kushibishwa na vitu vya dunia hii.
Upo utoshelevu wa mtu wa ndani, huyu mtu wa ndani hashibishwi na vitu vya kimwili, unaweza ukawa na kila kitu, ila ukaona kuna kitu hakipo sawa ndani yako.
Bila kuwa na uhusiano wa kweli na Mungu, tuwe na uhakika kiu yetu ya ndani itakuwa kubwa sana, kiu ikiwa kubwa itataka kupewa haja yake, ndipo utajikuta unaangukia mahali pabaya au pazuri.
Tunapaswa kujenga uhusiano mzuri na Mungu wetu, tunapaswa kumcha Mungu, tunapaswa kuwa na ibada na Mungu, mioyo yetu inapaswa kujaa neno lake, na sio kuwekeza nguvu zetu kutafuta mahitaji ya mwili tu.
Kufanya hivyo tutakuwa tumejiokoa na mambo mengi sana, tutakuwa vizuri kimwili na kiroho, lakini tukiwa vizuri kimwili, tuwe na uhakika anguko letu ni baya.
Marko 8
36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
Tafuta kwa bidii kuishibisha nafsi yako, elewa itakuwa ni hasara kubwa kuishi vizuri hapa duniani, alafu ukaikosa mbingu au ufalme wa Mungu.
Leo utasema acha nile maisha, ila utaingia hasara ya milele, bora kujenga uhusiano mzuri na Mungu wako, itakuwa faida kubwa sana.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana