Kitwanga: Serikali haipeleki maji Misungwi sababu inamuandaa Bashite Kugombea

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (CCM) adai serikali haipeleki maji jimboni kwake sababu inamuandaa Bashite kugombea

''Mbunge wa Misungwi (CCM) Charles Kitwanga alikwenda mbali zaidi na kutuhumu kuwa serikali haipeleki maji kwenye vijiji vyake kwasababu inamuandaa mtu aliyemtaja kwa jina la BASHITE kugombea ubunge kwenye uchaguzi ujao''

Mbunge wa Misungwi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi katika serikali ya awamu ya tano, Charles Kitwanga ameijia juu serikali na kusema kuwa inamhujumu ili apoteze jimbo katika uchaguzi ujao kwa kuamua kutokupeleka maji jimboni kwake.

Kitwanga alisema kuwa serikali imeamua kutokupeleka maji jimboni Misungwi kwa sababu wanamuandaa mtu anayeitwa Bashite kwenda kugombea katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Kitwanga aliyasema hayo jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambapo Waziri Mhandisi Gerson Lwenge aliliomba Bunge kuidhinisha TZS bilioni 672.2 kwa ajili ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Akichangia hotuba hiyo, Kitwanga alieleza hali ngumu ya upatikanaji wa maji wanayopitia wakazi wa kijiji cha Kolomije ambapo ndipo alipozaliwa Bashite.

Kuonyesha kukerwa na serikali kupuuza kupeleka mradi wa maji jimboni humo, Kitwanga alisema kuwa atahamasisha wananchi wa Misungwi kwenda kuzima mitambo ya maji ambayo ipo katika Kijiji cha Ihelele anachodai kuwa kimesahaulika katika miradi ya maji iliyopangwa kwenye bajeti ya 2017/28.

Kitwanga alisema kuwa wakati alipokuwa waziri alikuwa anashindwa kuibana serikali lakini kwa vile sasa ni mbunge tu, basi patachimbika.

Very unfair (si haki), nazungumza kutoka moyoni mwangu, haiwezekani mradi unakwenda Tabora unatumia 600 bilioni alafu watu wangu wanakosa maji hata ya bilioni 10, alisema Kitwanga.
 
Tusikubali ulaghai wa wanasiasa, Kitwanga ni rafiki wa Magufuli, alishindwa vipi kulisemea jimbo lake kwenye kikao cha baraza la mawaziri?

Nawashauri Watanzania wote wenye masikio na wasikie, mtu kama alishindwa kuwa msaada kwa jimbo lake alipokuwa waziri huyo hafai hawezi kuwasaidia lolote akiwa back bench. Piga chini.

Pamoja na upumbavu wote wa Bashite akijirekebisha tabia zake chafu ni aina ya mtu anayeweza angalau kuonesha alifanya hiki jimboni ingawa mimi kama Matola hata uniwekee bastora kichwani ni bora nife tu kuliko kumpigia kura jambazi aina ya Bashite.
 
Kwani si mara ya pili analisemea hili jambo. Ile mara ya kwanza iliishia wapi.?
 
Anaanza kutafuta mchawi kabla 2020!
Walevi wanatabia ya kutokupiga kura!
 
Tusikubali ulaghai wa wanasiasa, Kitwanga ni rafiki wa Magufuli, alishindwa vipi kulisemea jimbo lake kwenye kikao cha baraza la mawaziri?

Nawashauri Watanzania wote wenye masikio na wasikie, mtu kama alishindwa kuwa msaada kwa jimbo lake alipokuwa waziri huyo hafai hawezi kuwasaidia lolote akiwa back bench. Piga chini.

Pamoja na upumbavu wote wa Bashite akijirekebisha tabia zake chafu ni aina ya mtu anayeweza angalau kuonesha alifanya hiki jimboni ingawa mimi kama Matola hata uniwekee bastora kichwani ni bora nife tu kuliko kumpigia kura jambazi aina ya Bashite.
laiti kama Bashite asinge kubali kutumika kutaka kuua upinzani na kuweka pembeni tamaa za maisha ya kifahari hakika angekuwa ni kijana wa kuigwa ktk harakati za kisiasa. Ila mungu mkubwa kupitia yy tumeonyeshwa sura halisi ya mkulu iliyokuwa imejificha kweli mungu anawapenda watanzania.
 
Back
Top Bottom