Kituo cha Ubungo Bus terminal Kimehamia Simu 2000

Egwugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,558
Reaction score
8,552
Jamani mliobahatika kufika kituo kipya kutoka Ubungo kuamia sim 2000 waliofika hapo kituoni leo tupeni habari yake kwa harakaharaka mpangilio ukoje wa mandhari
========================

 
1. Jina la simu 2000 limetokana na nini kwanini kituo kisijulikane kama mawasiliano

2. Kuboresha kituo kuendane na uboreshaji wa barabara na mifereji ya maji kwakuwa eneo hilo huwa na kero nyingi sana kipindi cha masika kutokana na maji kutotiririkia bondeni na badala yake yanajaa barabarani
 

namba 2 nice observation mkuu! waangalie sana kuhusu hilo maana eneo liko chini na huwa hapafai hapo kipindi cha mvua kubwa. isje baadae kuwa kero.
 
Hili jina litawasumbua wapiga debe... Ubungo..Ubungoo...! Ilikuwa rahisi....Lakini Simu elfu mbili Simu elfu mbiliiii..!! wala hainogi.....Labda wafupishe...Sim... Sim...Simuuuuu...!!

Kutoshirikishwa wadau ni jadi ya watawala wetu.

Nadhani hili jina la simu 2000 halitakuwa famous hata kidogo.
 
Dah darajani palikuwa panaboa sana pale. Ila nchi hii, baada ya miaka mitatu watakihamisha tena.
 
Hili jina litawasumbua wapiga debe... Ubungo..Ubungoo...! Ilikuwa rahisi....Lakini Simu elfu mbili Simu elfu mbiliiii..!! wala hainogi.....Labda wafupishe...Sim... Sim...Simuuuuu...!!

Hahahah mkuu mbona unawatetea wapiga debe hivo au na ww ndo shughuli yako nini?
 
yani hawa jamaa wanazidi kufanya maisha kua magumu juu ya usafiri wa uma.
Na nitoe angalizo naona wanazidi kukuza kituo cha river side darajani hasahasa kwenye zile eneo la tanesco transfoma. hivi unategemea dereva atokae tabata au buguruni au gogo la mboto atakua na muda wa kusubiri taa ziwake ndio aende huko kwenye hizo simu zenu? labda kama na wao mnawawekea kituo hapo river side otherwise ni mwendo wa "kukunja chapati" kuwaongezea majanga abiria watokao mwenge kwenda uelekeo wa barabara ya mandela.
 
Afadhali. Sasa nitakuwa napitia njia yu ubungo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…