Mimi ni mwananchi ninayeishi maeneo ya Tabata Mawenzi, na napenda kuwasilisha yangu yalio machache kuhusiana na huduma za Tanesco yanayotolewa na kituo cha Tabata- Liwiti ,Mkoa wa Ilala. Binafsi nilikuwa nasikia malalamiko ya watu mbalimbali kuhusu huduma mbovu na zenye viashirio vya rushwa za Tanesco.
Mimi binafsi nina matatizo na LUKU ambayo iliharibika tangu tarehe 22/05/2014, niliwaatarifu Tanesco siku hiyo hiyo kwenye saa kumi na mbili jioni kupitia namba za hapo Tabata Liwiti za dharura, lakini hawakuja kwa wakati hadi nikaenda tena pale ofisini kwao kutoa tena taarifa, na hiyo ilikuwa kesho yake tarehe 23/05/2014 nayo haikuwafanya waje kutembelea sehemu ya nyumba yenye tatizo.
Nikiwa nakwenda pale ofisi za huduma za wateja, nilimkuta mdada mmoja nae hakuwa na lugha ambayo inapaswa kutolewa kwa wateja, yaani lugha ya kumsikiliza mteja kwa kueleza shida yake hadi amalize kuelezea shida yake ndio uulize maswali kwa kadiri inavyofaa lakini yeye hakufanya hivyo, inaonekana hana mafunzo na haelewi majukumu yanayomweka pale, na hii imejionyesha kwa wafanyakazi karibia wa ngazi zote ambazo nilikuwa napitia isipokuwa kuna mama mmoja huwa anasimama kwenye meza ya LUKU dept, inaonekama kama ndio Meneja mwenyewe, kwa sababu anajua jukumu lake na wale watendaji wanamsikiliza kwa kila jambo analolisema nakutoa malekezo.
Nikiendelea na ufutiliaji wangu wa Kurekebishiwa tatizo langu, nikawajulisha tena kupitia dirisha la huduma kwa wateja mara hii nikapewa namba nyingine(yaani TB Namba) ukizingatia pale mwanzo nilishapewa na niliwaambia namba yangu ni fulani na ninayo lakini yule dada wa pale huduma za wateja akawa anasisitiza niandikishe upya na nipewe namba nyingine ,ile ya mwanzo haioni,hii ilikuwa tarehe 26/05/2014.
Kwenye saa tano usiku wa tarehe 27/05/2014 mafundi wa dharura wa Tanesco-Tabata Liwiti wakafika nyumbani na wakaiangalia ile mita ya LUKU na kusema inafaa kubadilishwa na wakanishauri niende tena kwenye ofisi za Tabata –Liwiti kwa maelekezo zaidi.
Zoezi la nenda rudi lilinichukua zaidi ya miezi nne na mwisho kwenye tarehe 29/08/2014 niliambia ya kuwa ukitaka kufungiwa LUKU leo unabidi uchangie usafiri wa bajaj wa kuwaleta wafanyakazi watatu wa Tanesco nyumbani kuja kufunga hiyo na huo usafiri wanasema ni shs 10,000/=, mimi najiuliza je suala ili rasmi au ni wao wanajinufaisha kuwaibia watanzania masikini kama sisi tunalipa malipo bila kuwa rasmi ,ningeomba Tanesco watoe tamko rasmi kwa wananchi ya kuwa kuna huduma ya kulipia usafiri pindi watakapopata matatizo yeyote kwa wakati muafaka na waweke matangazo kwenye ofisi zao ili ijulikane hivyo,itapunguza maswali tunayojiuliza sasa,na tueleweshwe haya malipo kwa nini yanafanyika ili umma ujue.
Jambo lingine ambalo linawahusu wafanyakazi wake wengi, wawe wanatoa maelekezo kwa watumiaji wa umeme kwenye vifaa vyao, utakuta wanakupa karatasi (manual) ambazo zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza na maelezo hayatoshelezi, kwa mfano mimi sikujua kama LUKU zinakuja na units 50, nimekuja kugundua baadae sana,kwa sababu tu sikupata maelezo yaliyosema hivyo, hao mafundi wakija ni mbio mbio hawana hata muda,na makatasi mengine wanakurushia.
Na vile vile wawe wanaweka matangazo yatakayokuwa yanaonyesha muda wa huduma kwa wateja na ukibadilika watangaze kwenye baadhi ya sehemu za ofisi au watumie ofisi za serikali za mitaa ili umma utambue, mfano siku za nyuma nilikuwa naenda ofisini pale Tabata kwenye saa moja na Napata watu washaanza kazi na wanawahudumia watu,lakini juzi nikmekuta tofauti nimeenda muda huo huo yaani saa moja asubuhi lakini nikaambiwa ofisi zinaanza kuhudumia kuanzia saa mbili,kumuuliza yule afisa usalama pale getini haukweza kutoa jibu lenye ufasaha,alichosema labda waliwaweka mkisubiri,lakini mimi nilikuwa nawahi muda wa saa mmoa na kupata huduma.
Ninachosema ni kuwa mazingira haya yote yanaonyesha ofisi ufanisi wake si wa kuridhisha kuanzia kwa afisa usalama, mtoa huduma kwa wateja, mafundi wa dharura na mafundi wa idara ya LUKU,na hii inapelekea kuweka mazingira ya rushwa na kumkosesha huduma mteja za msingi kwa ajili ya manufaa yao binafsi.
Asante
Mwananchi Mpenda Haki - Tabata