Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Kwanza ieleweka kwamba ni jambo la msingi kwa usafiri wa jiji (commuter system) kuunganisha abiria na vituo vya aina mbalimbali za usafiri: Barbara, Reli, Maji, Anga, na chini ya ardhi. Hii ndio sababu wakoloni walijenga reli kuanzia bandarini na kuishia bandarini (Dar-Kigoma/Mwanza. Vivyo hivyo Mombasa-Nairobi/Kisumu etc.)
Halafu Commuter Bus Station ya zamani ilijengwa pale eneo la stesheni ya reli Dar, na bado ipo hadi leo ingwa nafasi sasa ni ndogo sana.
Kwahiyo hawa wataalamu wetu walipaswa kuzingatia hili kwanza. Kwasababu kwa mfano, abiria wa treni kutoka bara anaetaka kuunganisha kwenda Zanzibar au Lindi/Nairobi/nk. apate usafiri anaohitaji hapohapo karibu na stesheni ili kupunguzia bughudha za kukodi taxi au bajaji kumpeleka mbali kama Ubungo kwenye stendi ya mabasi ya mikoani. Huyu anaweza kuwa mgeni halafu ana watoto au mizigo nk.
Bahati mbaya sisi tunazidi kuongeza umbali kati ya usafiri wa mbali (reli na bus) na stesheni ya usafiri wa ndani (Simu commute bus station).
Abiri katoka Zanzibar au Kigoma akishuka stesheni/bandarini Dar lazima abadili bus kati ya mijini na Ubungo au Simu hata akipnda DART/UDA lazima abadili usafiri au atashuka mbali na lengo lake au kiunganishi cha safari yake.
UBUNIFU WA WATAALAMU
Pale ilipo atesheni ya reli, kwa ubunifu kilikuwa na nafasi ya kujenga complex ya kuunganisha reli na commuter system+bandari na mikoa. Lakini badala yake tumeuza maeneo ya ardhi ya railways ambayo yangetumiwa kwa kujenga complex ya aina hiyo kuanzia stesheni penyewe, Karakana, Gerezani, Shaurimoyo, Kamata nk.
Halafu tumehamisha mabasi ya mikoa kutoka Mnazimoja na Kisutu kwenda Ubungo na back tunapanga kuyapeleka Mbezi! yani iwe mbali zaidi kutoka Railway stesheni na Bandar! Jamani!
Hebu niishie hapa kwanza ili nipate mrejesho wenu ikiwa mnaliona hili.