Kituo cha kurekebisha tabia za Wanadamu

Kituo cha kurekebisha tabia za Wanadamu

Heaven Seeker

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2017
Posts
479
Reaction score
1,079
Mwanadamu ni kiumbe anayepaswa kuwa na tabia njema katika jamii anayoishi.

Mtoto anatakiwa kuwa msikivu, mwenye heshima, adamu na utii kwa wazazi na walimu wake. Anatakiwa kupenda shule na kujifunza mambo mbalimbali anayofundishwa na walimu wake.

Familia za watu zinatakiwa kuwa na Amani na Upendo. Mafarakano katika ndoa na maisha ya kawaida siyo sifa ya Mwanadamu aliye katika hali ya kawaida.

Matendo mabaya kama vile wizi, ubakaji, ulevi wa kupindukia n. k siyo sifa ya Mwanadamu aliye kamilika.

Mtu kuwa na roho mbaya, kutopenda kutoa misaada kwa ndugu na jamaa kama amejaaliwa kuwa na nafasi hiyo, uchoyo, ubinafsi na ugomvi wa aina yoyote ile siyo sifa kabisa ya Mwanadamu aliye katika hali ya kawaida.

Ubinafsi, kujipenda mwenyewe, kulipiza visasi, uchonganishi, kiburi, dharau, jazba na kujikweza siyo tabia sahihi za Mwanadamu wa kawaida.

Jamii yetu kwa sasa imejawa na watu wenye sifa nyingi nilizotaja hapo juu. Ukienda maofsin na maeneo mengi ya kazi utakutana na watu wenye tabia hizo.

Ukienda mashuleni utakutana na watoto wasio na adabu, wasiopenda shule na tabia nyingi mbaya kama hizo.

Kwa bahati mbaya sana, hata kwenye nyumba zetu za Ibada siku hizi utakutana na watu wa aina hiyo. Si umewahi kusikia Mchungaji, Padre au Askofu fulani wa mahala fulani amepata kashfa hii na ile.?

Makanisani na kwenye nyumba nyingine za Ibada ilitakiwa kuwa mahala muhimu ambapo watu wanaweza kubadilishwa tabia zao mbaya na kuwa na tabia nzuri zinazofaa. Lakini cha ajabu utakutana na mamia ya watu wanahudhuria vizuri makanisani na nyumba nyingine za Ibada lakini tabia zao haziakisi matendo mazuri kwenye jamii wanayoishi. Kwa ufupi ni kuwa, nyumba za Ibada imekuwa mahala pa mazoea ambapo watu huenda kutimiza mila na desturi za jamii anayoishi.

Sisemi kuwa Mwanadamu anaweza kuwa mwenye tabia nzuri kwa asilimia mia moja, lakini angalau tunataka ukimuona mtu useme kweli mtu huyu ni mwema, mtu huyu ni kimbilio la wanyonge, mtu huyu ni msikivu mwenye kujali watu na mwenye huruma, mwenye kufariji wenye mahitaji na mkarimu wa rohoni na mwilini.

Tufanye nini sasa.?

Bado sisi wanadamu tunaweza kuibadilisha jamii yetu. Ikaachana kabisa na mambo yasiyofaa na kutenda yanayofaa.

Ndipo wazo la kuanzisha kituo cha kurekebisha tabia lilipoanza.

Hiki ni kituo maalumu ambacho watu watajiandaa kuishi vizuri katika jamii yao. Watu wataleta vijana wao wajifunze kuishi maisha ya ndoa bila ya mafarakano mengi.

Watu wataleta vijana wao wanafunzi kurekebishwa tabia pale inapoonekana wanatabia zisizofaa.

Waajiri watawaleta wafanyakazi wao kujifunza kufanya kazi kwa bidii, upendo, kujituma, nidhamu nzuri na kuwa na maadili mengine mazuri katika kazi.

Watu watawaleta ndugu zao walio wezi na vibaka kubadilishwa tabia zao na kuwa watu wenye tabia njema.

Watu watawaleta vijana wao wanaohitimu masomo yao na kujiandaa kuanza kuishi maisha ya uraiani ili wafundishwe kanuni za maisha bora Duniani.

Watu watawaleta jamaa zao wanaoonekana kukata tamaa ya maisha na kuishia kuwa na tabia zisizofaa katika jamii. Kisha watu hawa watabadilishwa tabia na kuwa watu wema.

Watu watafundishwa namna sahihi ya kuishi.

Huwezi kutenganisha mbinu za kumfanya mtu kuwa mtu mwema na imani za Dini zetu ila kituo hiki hakitakuwa cha Kanisa wala Msikiti.

Wachungaji, Masheikhe, Maimamu, Mapadre, Maaskofu, Wanafalsafa, Wanasaikolojia, Wachumi na Madaktari wa Afya ya mwili watakuwa walimu wa kituo hiki. Watapata nafasi ya kufundisha kwa kujitolea na kujipatia ujira pia.

Ndugu jamaa na marafiki watawaleta ndugu zao kwa kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya kuendeleza kituo hiki. Mwanafunzi katika kituo hiki atahudhuria masomo au vipindi kwa mpangilio maalumu kwa muda wa siku kadhaa kulingana na uhitaji wake na uwezo wake wa kugharamia masomo.

Na hii ndio ndoto niliyoota leo usiku kuwa nimeanzisha kituo hiki baada ya miaka miwili ijayo.

Japokuwa ni ndoto, ila nimeanza mikakati ya kutekeleza ndoto hii.

Wewe una maoni gani juu ya ndoto hii.?
 
Ukachukue skills pale jitegemee!
 
Jiwe asikosane kwenye hicho kituo

Na Mtoto ake bashite stone !
 
Wazo zuri,anzisha linawezekana japo changamoto zitakuwepo,familia nyingi zimeshindwa kuwaanda watoto juu ya taratibu za maisha,pengine wanazidiwa na majukumu ya kiuchumi, wanapenda kizazi chenye maadili lakini wameshindwa kuwaadilisha.
 
Kabla ya wewe kufikilia wengine walikuwa na hilo wazo.

Mimi binafsi nimekuwa na wazo hilo but linebobea kwenye pande zaidi ya ulizotaja hapo, nilijifunza hurka za watanzania (WAKATISHA TAMAA) unapoongea naye mfanye jambo kama hili anakuuliza utanilipa shs ngapi 😔!!.

Otherwise karibu tujenge Taifa.
 
Wazo zuri,anzisha linawezekana japo changamoto zitakuwepo,familia nyingi zimeshindwa kuwaanda watoto juu ya taratibu za maisha,pengine wanazidiwa na majukumu ya kiuchumi, wanapenda kizazi chenye maadili lakini wameshindwa kuwaadilisha.
Nashukuru sana. Umenitia moyo na nguvu.

Jamii yetu inapenda watu wema, ila haija-invest vya kutosha kutengeneza kizazi chema.

Vyuoni tunafundishwa utaalamu wa kurusha ndege, utaalamu wa kutengeneza meli na ndege, ujuzi wa wanyama na mimea na mambo mbalimbali kama hayo. Ila elimu ya maisha mema imekuwa nadra kuipata.

Kwenye nyumba za Ibada watu hawaendi tena kujifunza na hakuna commitment ya viongozi wa Dini kuwa lazima watu wabadilike, isipokuwa imekuwa ni mahala pa kutekeleza mila na desturi za maisha yetu.
 
Kabla ya wewe kufikilia wengine walikuwa na hilo wazo.

Mimi binafsi nimekuwa na wazo hilo but linebobea kwenye pande zaidi ya ulizotaja hapo, nilijifunza hurka za watanzania (WAKATISHA TAMAA) unapoongea naye mfanye jambo kama hili anakuuliza utanilipa shs ngapi !!.

Otherwise karibu tujenge Taifa.
Mkuu, umoja ni nguvu.

Ukikutana na mtu mwenye mtizamo sawa na wako ni rahisi kufanikisha jambo. Karibu.
 
Ni wazo zuri sanaa!!! Pambania ndoto yako uitimize, maana itasaidia jamii kwa kias kikubwa
 
Ni wazo zuri sanaa!!! Pambania ndoto yako uitimize, maana itasaidia jamii kwa kias kikubwa
Nashukuru kwa kunitia moyo. Nina maono ya kufanikisha ndoto hii baada ya miaka miwili. Yaani kuanzia 2021/2022.

Kwa sasa naanza kuandaa miundombinu ya roho, mwili na mfukoni. Maana ukihitaji kumnyanyua aliyekaa, unatakiwa wewe kwanza uwe umesimama ndipo utapata urahisi wa kumnyanyua.
 
Back
Top Bottom