chrispin Manyeresa
New Member
- May 26, 2013
- 3
- 1
Habari za muda huu wadau, Natumaini tunafanya vyema kazi ya kulijenga taifa.
Nimejiuliza sana kuhusu kituo chetu cha haki za binadamu Tanzania ( LHRC) je kipo katika mrengo gani kutokana na kwamba ninaona kinajikita zaidi kutetea haki za kisiasa na diplomasia, je ndio kazi yake?
wanafadhaliwa na watu gani? yote haya ni maswali ambayo nimekua nkijiuliza sana na kukosa majibu yake, ni kwanini hakijajikita na sana na mambo husika zaidi ambayo nadhani kingeweza kuifanya serikali ikafuatilia. Ni nini kinachofanya mpaka kituo hiki kutokua na hulka ya kutetea haki za binadamu kama kinavyoitwa?
Kumekua na matukio ya kutisha nchini mwetu na naweza kusema ndan ya mwezi huu wa Mei tu matukio ya kufanya mauwaji kwa njia ya kuchinja watu kama kuku yamepoteza watu si chini ya 20, na pia ni swala ambalo sio dogo katika masikio ya watu wanaotambau utu na haki ya mwanadamu kuishi.Je kituo hiki hakioni haya yanayoendelea nchini. Kwanini kisiihoji serikali kwa swala hili kuendelea kufumbiwa macho kana kwamba watu wanaopeteza maisha si wanadamu au kama kimeshindwa basi ni vyema kujibadili jina ili ifahamike kinatetea haki za wanasiasa tu pale wanapoonekana kuonewa na serikali.
Watu wanachinjwa kila juma na serikali imekua ikifumbia macho na kituo hiki kilitakiwa kuonesha msimamo wake kutetea kumwagwa kwa damu zisizo na hatia za Watanzania hawa.Kituo hiki kinauwezo wa kuisukuma serikali kufanya kazi yake katika swala zima la usalama wa raia na mali zake kwanini hakiongelei hayo?, kwanini kinaacha mambo amabyo ndio lengo lake kuu la kuanzishwa? Tumekua tukishuhudia kituo hiki kikitoa matamko magumu kwenye maswala ya siasa hata kufukia hatua kuingialia muhimili mkuu wa serikali yan bunge pale kinapotoa amri wabunge kadhaa walio fungiwa kwa mda kurudishwa bungeni wakati mamlaka hio hakina hata mahakama kuu ya nchi haina mamlaka ya kuingilia bunge.
kwanini kisijikite kwenye maswala ambayo yanaendelea hivi sasa. Hali ya usalama wa wananchi wa mkoa wa Tanga si shwari kituo hiki kimekaa kimya kabisa. Sasa ni wakati wa kituo hiki kuangalia mambo ya msingi zaidi kwenye usalama wa wananchi pale wanaponyanyaswa.
Naomba kuwasilisha Asante