Sango Ochwera
Member
- Mar 20, 2013
- 98
- 26
Wakati wananchi wilayani Rorya mkoa wa Mara wakiendelea kuvuta subira kuelekea maisha bora kwa kila mtanzania,hali ya huduma za afya wilayani humo inazidi kuwa mbaya kila kukicha.
Kituo cha afya cha kata ya Rabuor Tarafa ya Luo imbo ambacho kinahudumia wakazi wapatao 13626 kutoka vijiji vya makongoro,rabuor na oliyo hakina dawa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.
Sambamba na ukosefu huo wa dawa,kituo hiki hakina wataalamu kama clinical officer(co),nurse,labaratory technician na assistant labaratory technician.Kutokana na hali hiyo wananchi wanaofika kituoni hapo kupata matibabu husikilizwa maelezo yao na kisha huandikiwa dawa na kutakiwa kwenda kununua.
Aidha kituo hiki cha afya kina upungufu mkubwa wa samani kiasi cha wahudumu wachache waliopo kutumia madumu ya mafuta ya kula ya ujazo wa lita 20 kama viti.
Source:mimi mwenyewe.