Kitunguu swaumu kinazuia influenza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitunguu swaumu kinazuia influenza!

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jan 30, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Kitunguu swaumu tangu kale kimekuwa kikijulikana kama 'dawa ya kushangaza' na kutumiwa na watu wengi katika kutibu mafua na influenza. Miongoni mwa faida za kitunguu swaumu ni kuzuia kupatwa na magonjwa mbalimbali na maambukizo ya virusi. Hivyo kitunguu swaumu hujulikana kama antibiotiki ya asilia. Uchunguzi umeonyesha kwamba kula kitunguu swaumu kunapunguza kushadidi ugonjwa wa influenza na hata kuzuia kupatwa na ugonjwa huo. Vilevile kula kila mara kitunguu swaumu, huzuia kupatwa na magonjwa ya moyo, kwani kitunguu swaumu huzuia damu isigande kwenye mishipa ya damu.
  Halikadhalika kitunguu swaumu ambacho pia ni kiungo muhimu cha chakula kina potassium, na hivyo watu wenye ugonjwa wa shinikizo la damu wanashauriwa kula vyakula vilivyopikwa kwa kitunguu swaumu.
  Si vibaya kujua kuwa katika uchunguzi uliochapishwa mwaka 2001, imeelezwa kwamba, kitunguu swaumu kina athari kubwa na nzuri pale kinapochanganywa na baadhi ya dawa nyinginezo katika kutibu Ukimwi au HIV.
  Haya shime jamaniĀ… kuanzia leo vyakula visikose kuungwa na kitunguu thomu, iwapo unaogopa kupatwa na influenza kama mimi!
   
 2. 2my

  2my JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya mzizimkavu 2mekupata!!!!!!sisi tu sasa na hicho kiungo
   
 3. Kimori

  Kimori JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2010
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupe tena dawa nyingine!
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jan 31, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ukijuwa kula kitunguu swaum, ujuwe na kusafisha kinywa.
   
 5. a

  ambu Member

  #5
  Jan 31, 2010
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  ahsante kwa kutukumbusha kula thaumu
   
Loading...