sambusa zinakifu, nyingi zina uchafu
zinapikwa kwa rafu, kipato kijidurufu
zimepunjwa minofu, ukiziona dhoofu
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua
Bora kusifu andazi, lipikwalo kwa uwazi
Ndani latiwa nazi, ladha kuipalizi
Ulishawekwa uwazi, Kitumbua si andazi
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua
Ukisema cha Mchanga, Utakuwa na kilanga
kosa la mkaanga, hata sambusa unangwa
Kitumbua kinakonga, waweza hata kuonga
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua
Sambusa kwa pilipili, mtoto katu haili
Na kusema ukweli, kitumbua ndio dili
Ukipata tu viwili, njaa inajighaili
Malenga nawaambia, hakuna kama kitumbua
(c) Funzadume (Soli ya Mbingu) mwana wa washawasha 2010