Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,229
KITU CHA KUFANYA PALE WATU AMBAPO HAWAKUAMINI KAMA UNAWEZA KUFANYA
Kama unataka kufanya jambo jipya, kama unataka kufanya jambo
tofauti na wengine walivyozoea kufanya, naweza nikakuhakikishia jambo moja, WATU HAWATAKUAMINI.
Watu hawatakuamini kwamba unaweza kufanya jambo hilo.
Watu hawatakuamini kwamba kuna uwezekano wa jambo hilo kufanyika kwa tofauti.
Na hapa ndipo watu wengi hukata tamaa na kuamua kuacha. Na hivyo watu wale walioshindwa kuwaamini mwanzo wanakuwa sahihi na wanazidi kupata nguvu ya kuwaambia wengine kwamba hawawezi au haiwezekani.
Leo nataka nikuulize, je unajua unatakiwa kufanya nini pale ambapo watu hawakuamini kwamba unaweza?
Au umekuwa mtu wa kukatishwa tamaa mara nyingi na wewe kukubali?
Sasa kuna kitu kimoja muhimu sana unachotakiwa kufanya pale ambapo watu hawakuamini kama unaweza.
JIAMINI WEWE MWENYEWE.
Wewe ndio umekuja na mawazo hayo uliyonayo, wewe ndiye ambaye umekuwa unafikiria usiku na mchana jinsi unavyoweza kubadili hali ya mambo. Wewe ndiye uliyefikiria na kuona kuna njia mbadala na ambayo inawezekana.
Sasa kwa nini ukubali kumsikiliza mtu ambaye amefikiria kwa upande mmoja tu wa kwamba vitu haviwezekani?
Kama utawasikiliza watu hawa utakuwa hujajitendea haki kabisa,
kwa sababu hata watu hawa sio kwamba wana uhakika haiwezekani, ni vile tu hawajawahi kuona mtu mwingine akifanya hicho unachotarajia kufanya.
Kama watu hawaamini kwamba unaweza, huo ndio wakati wa kujiamini
na hata kufurahia sana kwenye maisha yako. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu
unapoanza kufanya kitu ambacho wengi wanaona hakiwezekani, jua unafanya kitu
ambacho sio cha kawaida, unafanya kitu kikubwa.
Na mafanikio yanakuja kwa kufanya vitu ambavyo sio vya kawaida.