Kitovu chako kilitupwa wapi?

Kitovu chako kilitupwa wapi?

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
286
Reaction score
599
Utangulizi

Kitovu ni ishara ya nje ambayo inaonyesha muunganiko wa mtoto na hasili yake.

Ezekieli 16:3-4
[3]useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti.
.
[4]Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.

Mungu anasema na Yerusalemu habari ya Kuzaliwa kwake ,anawataja wazazi wake yaani nchi zile ambazo Yerusalemu walizichukua kuwa nchi Yao ndio wanaitwa wazazi na anasema asili ya Yerusalemu haikuondolewa na ile nchi ambayo Mungu aliwapa ndio maana Maisha Yao yalikuwa sawasawa na ile nchi ambayo aliwapa

Kumbukumbu la Torati 20:17-18
[17]lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru BWANA, Mungu wako;

[18]wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya BWANA, Mungu wenu.

Mungu anasema na Yerusalemu ambaye ni Mimi na wewe kwamba Maisha Yao yanatokana na tabia za wazazi wao kwa sababu wazazi wao ambao ni wakanaani na waamori ni watu ambao walikuwa wakiabudu Mungu mingine ndio maana anaona vitendo vya watoto wake vinatokana na nchi ambayo walipokea urithi ambao Mungu aliwapa

Mungu anatumbia kwamba kitovu linatengeneza Hatima ya Maisha yetu , anasema aliona tabia ya kuabudu Miungu migeni kutoka kwa watoto wake Israeli itokana na kurithi nchi ambayo walikuwa ni waabudu Miungu akielezea Kwa picha ya mtoto ambaye amezaliwa na wazazi ambao wanaabudu Miungu migeni lakini wakati anazaliwa kitovu chake hakikukatwa katika jinsi ya Rohoni ili asiweze kuendelea kuitumikia Miungu ya wazazi wake.

Swali langu kwako ,unajua baada ya wewe Kuzaliwa kile kitovu chako walipeleka wapi ? Ulishawai kuumuuliza Bibi, shangazi , mama mkwe au Baba mkwe kile kitovu cha mtoto wako alikipeleka wapi ?

Je unajua kitovu cha mtoto wako au chako mwenyewe ni lazima kikatwa katika ulimwengu wa Roho ili wewe usiwechini ya utawala wa Miungu ya wazazi wako?

Ulishawai kuuliza juu ya asili yako , uko nyuma hapo zamani walikuwa wanapeleka wapi vitovu vya watoto?

Karibu tuchangie.
 
Umeshawai kujiuliza , unamuuliza mzazi anakwambia wakati ukiwa mtoto kitovu chako na nywele zako za Kwanza zilifungwa kwenye kitambaa cheusi na ukafungwa kiunoni kwa ajili ya ulinzi?

Ushaujiuliza huo ndio ulinzi gani? Ambao unazungumziwa maana Kwa kawaida uwezi kulindwa kwa kutumia kitovu na nywele kama ulinzi , inamaana kuna ulinzi wa kiroho

Ni roho gani inayotawala ? Mungu wetu katika Kristo atoa ulinzi kwa njia ya mafundo , inamana unapewa ulinzi na mizimu


Sasa umepewa ulinzi kutoka kwa mizimu alafu Leo unasema umehokoka wakati ujakata agano na mizimu Kwanza ili Mungu akusaidie.

Ni kweli ni Mkristo lakini wewe kila unapokwenda haupati kibali unajiuliza kwanini?

Unapataje kibali wakati bado mizimu ya kwenu ina uhalali na Maisha yako, ulishawai kujiuliza kwanini kila unapokwenda wewe unakataliwa kwa sababu bado uko kwenye umiliki wa Miungu
 
Kitovu ni masalia ya sehemu ya mwili iliyokuunganisha na mama yako ukiwa ndani ya uterus.

Tuache kupeleka kila kitu kiimani.
 
Back
Top Bottom