KITINE-naunga mkono maandamano ya CHADEMA

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Kitine: Utajiri wa wachache Tanzania ni hatari kwa usalama Send to a friend
Wednesday, 29 June 2011 20:35
0digg

kitine%20faidika.jpg
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Serikali ya awamu ya kwanza Dk Hassy Kitine, akizungumza Dar es Salaam jana na washindi wa shindano la shinda 'Nina Ndoto' linaloendeshwa na Kampuni ya Faidika. Picha na Emmanuel Herman

Mwandishi Wetu
ALIYEWAHI kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Serikali ya awamu ya kwanza Dk Hassy Kitine amesema hali iliyopo sasa nchini ya umaskini mkubwa kwa wananchi inatishia amani.

Kitine ambaye aliwahi pia kuwa mbunge amesema taifa haliwezi kuwa na asilimia moja pekee ya watu wanaoshikilia uchumi wa nchi kama ilivyo sasa Tanzania huku asilimia 99 wakiwa mafukara.

"Watanzania wengi ambao ndiyo wenye nchi hii wanamiliki uchumi kwa asilimia moja tu, huku Watanzania walio chini ya asilimia moja kwa wingi wao wakimiliki uchumi kwa asilimia 99,"alisema Kitine na kuongeza:

“Hali hii inatisha na ni hatari kwa kundi dogo la watu wachache kumiliki uchumi wa Watanzia kwa asilimia 99.“


Mbele ya wanahabari Kitine alisema, "Mnajua napenda kusema, lakini nikisema wengine wanakasirika. Lakini, lazima tusema, Watanzania wengi lazima wamiliki uchumi kikamilifu na si watu wachache."

Akijibu swali kuhusu maandamano yanayoendeshwa na Chadema kupinga hali ngumu ya maisha nchini alisema anakiunga mkono chama hicho akisema kiko sahihi katika kufanya maandamano hayo.


"Hali hiyo ni kitu ambacho kizuri na kinaleta changamoto kwa ‘political parties’ (Vyama vya siasa) na viongozi, kwani hawawezi kufanana, maandamano ni mazuri, ni demokrasia, japo mimi ni mwanachama wa CCM," alisema Kitine.
Akizungumzia Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na kipindi cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Nne ya Jakaya Kikwete, Kitine alisema kwamba haoni tofauti katika vipindi hivyo viwili.
Hata hivyo, alisema mambo yamekuwa mabaya kutokana na kuondolewa kwa Azimio la Arusha na kwamba uongozi sasa umekuwa wa kununua.
"Zamani nilipokuwa kiongozi katika Serikali ya Awamu ya Kwanza baada ya kuteuliwa na Rais Nyerere kushika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Uwaziri na hatimaye Ubunge, uongozi ulikuwa ni ‘dedication’,"alisema.

Alifafanua, "zamani ukitaka kugombea nafasi ya uongozi kama ubunge unaulizwa mali umepata wapi, wenzako wataakuuliza, lakini nikaacha kugombea tena uongozi kutokana hali iliyojitokeza ambayo sasa uongozi unanunuliwa."

Kuhusu kampuni yake ya Faidika amesema hivi sasa inajishugulisha na kuwasaidia wafanyakazi wa sekta ya umma na hapo baadaye itaanza kusaidia pia watu wa sekta binafsi .

Kitime alikuwa akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la pili la ‘shinda ndoto yako’ linaloendeshwa na Kampuni ya Faidika inayojishugulisha na mikopo kwa wafanyakazi wa umma.

Kuhusu kampuni ya Faidika alisema hivi sasa inajishugulisha na kuwasaidia wafanyakazi wa sekta ya umma na hapo baadaye itaanza kusaidia pia watu wa sekta binafsi .

Katika hafla ya jana Mwalimu ya Shule ya Msingi Pongwe iliyopo mkoani Tanga Amiri Ligalwike alikabidhiwa Sh 5 milioni baada ya kuandika mchanganua wake vizuri kuhusu fedha alizokopa sh1.5 milioni jinsi alivyozitumia na kuweza kuboresha maisha yake ya kila siku na jirani zake.
Mshindi mwingine ni Makono Andrew aliyeshinda Sh 3 milioni.


 
Wote wenye upeo wa kufikiria watarudi CDM magamba watabaki na magamba yao.Sema MZEE Kitine, tunajua hata udhalilishaji uliofanywa kwako kuhusu matibabu ya mama yetu enzi zile ulitokana na mbio za urais 2005 lakini baadae ukweli ulijulikana hasa baada ya wizi wa EPA uliofanywa na aliyejulikana kama MALAIKA nafikiri mzee unanipata
 
............................................A POEM BY NKUBA




MARCH WE IN LINES;
March we in lines​
Harmlessly, we no soldiers​
But disciplined:​
To face our common foe​
Our arms are slogan on posters​
That annoys them, with the crown​
The furious murderous faces​
Trained to kill and detain:​
With fire arms and tanks​
We are not afraid of the whip and torture​
A thousand bullets with a million deaths​
We must die for the changes we aspire​
March we in lines bravely to face death​
And get what we most desire​
Though we know the first bullets will grant us death​
For this dirty life we lead​
Let the first bullet be upon my head:​
 
Back
Top Bottom