Kitilya, Sioi na Sinare warudishwa tena rumande mpaka Mei 3

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
kitilya1.jpeg

Aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare April 27 2016 walikosa dhamana kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa mahakama kuu kupinga maamuzi ya kupewa dhamana.

Leo April 29 2016 kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo awali Hakimu Mchauru alitoa maamuzi ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka Mei 12 mwaka huu, sababu ni kutokana na jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kukatwa kwa rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.

Muda mfupi baadae majira ya saa 4;30 asubuhi walirudishwa tena mbele ya Hakimu Mchauru baada ya kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam akitamka kesi hiyo itajwe Mei 3 mwaka huu badala ya mei 12, aliyoipanga awali.

Hakimu Mchauru amesema sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi itatajwa tena Mei 3 mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi yatabaki kama ilivyo, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
 
Nahisi kuna kuzidiana kamchezo kale ka mahakama zetu za awamu iliyopita. Kwa washtakiwa kama wataendelea kufaiti kwa mbinu zisizo halali, watafilisiwa kirahisi kabisa!
 
Aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare April 27 2016 walikosa dhamana kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa mahakama kuu kupinga maamuzi ya kupewa dhamana.

Leo April 29 2016 kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo awali Hakimu Mchauru alitoa maamuzi ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka Mei 12 mwaka huu, sababu ni kutokana na jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kukatwa kwa rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.

Muda mfupi baadae majira ya saa 4;30 asubuhi walirudishwa tena mbele ya Hakimu Mchauru baada ya kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam akitamka kesi hiyo itajwe Mei 3 mwaka huu badala ya mei 12, aliyoipanga awali.

Hakimu Mchauru amesema sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi itatajwa tena Mei 3 mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi yatabaki kama ilivyo, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
hapa ndio tutaona uhuru wa mahakama ndio nini. hakimu mfawidhi hapa anacheza kamchezo kachafu in favour ya hawa washtaliwa. kumlazimisha hakimu mwingine ndio uhuru wa mahakama. biashara ya kuuza haki ndio jipu kubwa sana.
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imesita kutoa uamuzi wa kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni kwa madai, jalada lake limeitishwa Mahakama Kuu, anaandika Faki Sosi.

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, hana mamlaka ya kutolea uamuzi wa kesi hiyo kutokana na jarada lake kuitishwa Mahakama Kuu leo asubuhi.

Kutokana na hali hiyo Hakimu Mchaura amesema kwamba, kesi itatajwa tena tarehe 12 Mei mwaka huu na watuhumiwa watarudishwa rumande.

Kitilya na wenzake leo walirudishwa tena mbele ya Hakimu Mchauru saa 4:30 baada ya hakimu kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akimtaka kesi hiyo itajwe Mei 3, mwaka huu badala ya tarehe 12 Mei mwaka huu aliyoipanga awali.

Hakimu Mchauru amesema, sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi itatajwa tena tarehe 3 Mei mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi yatabaki kama ilivyo.
 
Kwa hiyo sheria haifuatwi kwa sababu ni wachaga na wameru? Masikini huwa wanachuki za ajabu kweli
Sasa unafikiri ni nini?? We huoni wanaofanyiwa hivi vimbwanga ni wakaskazini pekee... Ule mkopo wa Billion 600 mbona hatuambiwi ulitumikaje na waliokula wanajulikana ila mpaka leo hawajafanywa chochote ila waliokula 1% ndio wanakamatwa
 
Hapo nimekuelewa mkuu, pole ni katika mapambano wakati mwingine mnaweza kujeruhiana wenyewe kwa wenyewe. Nimeipata mantiki yako
 
Kwani bado wanachunguzwa? ule ushahidi wa CFO hautoshi? maana ninajua sisi hatuwezi kuwa na uwezo wa kuchunguza na kuja na taarifa mpya zaidi ya zile zilizoumika kutoa hukumu huko London. Wapigwe miaka kadhaa tu mambo yaishe. Kupanga ni kuchagua. watafaidi mihela yao baada ya kutoka jela.
 
Back
Top Bottom