Kitila Mkumbo: Vyama vyote vikongwe vya siasa Tanzania,havina Demokrasia

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,629
34,173
KATIKA miezi saba ya utawala wake, Rais wetu mpya amefanikiwa kujipambanua katika mambo makubwa manne. Mosi, Rais amejitambulisha vyema kwa kauli na vitendo kwamba anaweza kubana matumzi ya serikali.

Katika kutekeleza hili amekuwa akichukua hatua kadhaa ikiwemo kufuta maadhimisho ya sikukuu za kitaifa kama vile maadhimisho ya Uhuru, Muungano na siku ya Ukimwi duniani.

Fedha zilizotengwa kwa ajili ya maadhimisho haya alielekeza zitumike katika miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa barabara.

Pili, Rais amejitambulisha kuwa kiongozi anayeamini kwamba tunapaswa kujiendesha kama taifa na hivyo amehimiza kulipa kodi. Taratibu wananchi wameanza kuelewa dhana na umuhimu wa kulipa kodi, na kwamba serikali haina miujiza ya kuleta maendeleo zaidi ya kukusanya kodi kutoka kwa wananchi.

Tatu, Rais amejitambulisha kwa kufufua ari ya kufanya kazi. Pamoja na kwamba hajajieleza kwa ufasaha sana katika eneo hili, lakini kaulimbiu yake ya Hapa Kazi tu imeleta hamasa mpya kuhusu umuhimu wa kufanya kazi.

Kauli mbiu hii na hotuba zake kadhaa zimekuwa chachu muhimu katika kuwakumbusha wananchi kwamba hakuna muujiza wa kuleta maendeleo nje ya kuchapa kazi kwa bidii na umakini.

Nne, Rais amejitambulisha kwamba ni kiongozi anayechukia ufisadi na amepania kupambana nao kwa vitendo. Katika kutekeleza hili amekwishafukuza watumishi wa umma waandamizi kadhaa waliotuhumiwa kufanya ufisadi tangu aingie madarakani.

Pamoja na kwamba mazingira na utaratibu wa kufukuzwa kwao umeacha maswali mengi na shaka kubwa juu ya azma ya Rais ya kuheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu, hatua alizochukua zimepeleka ujumbe muhimu kwamba ana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi.

Aidha, katika hili la kupambana na ufisadi Rais amekuwa jasiri kushinda chama chake ambacho katika Ilani yake ya mwaka 2015 kiliogopa hata kutumia neno ufisadi.
Hata hivyo, ujasiri wa Rais Magufuli ungetamalaki kama angeenda mbali kwa kutikisa mifumo ya kiutawala inayotafuna pesa nyingi za umma.

Kwa mfano, angefuta mbio za Mwenge ambao umuhimu wake uliisha mwaka 1992 mara baada ya nchi yetu kurudi katika mfumo wa vyama vingi. Pili, Rais angetikisa mfumo wetu wa utawala kama angefuta nafasi ya mkuu wa wilaya ambayo tafiti zote za sayansi ya siasa na utawala wa umma hapa nchini zimeonyesha kwamba, kwa mfumo wetu wa utawala wa sasa ndani ya mfumo wa vyama vingi, nafasi hii haina tija kwa taifa, na iliwekwa katika kufanikisha mfumo wa utawala wa kikoloni.

Umuhimu wake pekee umebaki kwa chama tawala kama njia ya kuwapa nafasi wanasiasa ambao wamekosa nafasi za uongozi na kazi katika chama chao na serikalini. Kwa kutekeleza kikamilifu azma yake ya kubana matumizi ya serikali tangu aingie madarakani, ingetarajiwa kwamba nafasi hii angeifutilia mbali kwa kutumia mamlaka aliyopewa kikatiba ya kuanzisha na kufuta nafasi katika utumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pengine ujasiri mkubwa ambao Rais Magufuli anaelekea kuuonyesha na ambao unaweza ukaja kuwa ndicho chanzo cha anguko lake ni katika kufifisha na hatimaye kuangamiza mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Inaeleweka kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) hawajawahi kuridhia kikamilifu uwepo wa mfumo wa vyama vingi kisiasa.

Waliwahamasisha wanachama wao na wananchi kwa ujumla waukatae mfumo wa vyama vingi wakati wa Tume ya Jaji Nyalali iliyokusanya maoni kuhusu mfumo wa siasa nchini mwaka 1990/91. Na katika hili walifanikiwa kwani ni asilimia 20 tu ya wananchi ndiyo walioridhia kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Aliyeokoa jahazi ni Mwalimu Nyerere kupitia hotuba yake kali aliyoitoa kwa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Mjini Mwanza mwaka 1990. Mwalimu Nyerere aliwaambia vijana wa CCM na chama chao kwa ujumla kwamba mfumo wa vyama vingi hauepukiki. Walinuna lakini wakawa hawana namna maana maoni ya Mwalimu Nyerere yalikuwa ni amri kuu kwa nchi.

Hivyo basi, viongozi wakuu wa CCM wamekuwa wakiishi na mfumo wa vyama vingi kinafiki kama njia ya kuwaridhisha wafadhili kutoka nchi za magharibi. Mfumo wa vyama vingi ni njia tu ya kuwadanganya wazungu ili waweze kuendelea kutupatia misaada lakini hawauoni kama njia halali ya kuchochea mawazo mbadala ya kisera na kubadilishana uongozi kwa amani kadri ya matakwa ya wapiga kura.

Ndiyo maana mfumo wetu wa uchaguzi umetengenezwakatika mazingira ya kuhakikisha unalinda ushindi wa CCM. Kwa hiyo watawala wanaona kwamba kazi pekee ya upinzani ni katika kutoa changamoto na maoni kwa chama tawala lakini sio kama serikali mbadala kadri wapiga kura wanavyoamua.

Hata hivyo Rais Magufuli inaelekea amepania kuachana na unafiki wa viongozi wenzake wa CCM waliopita. Hataki kukaa na mfumo wa vyama vingi kinafiki. Kauli zake zinaonyesha kwamba anataka mfumo wa vyama usiwepo kabisa, na ukiwepo pawe na vyama ambavyo havina athari katika utawala wake na ushindani wa kisiasa huko mbeleni.

Ndiyo maana ametangaza waziwazi kwamba hataki siasa hadi mwaka 2020,na sasa serikali yake imepiga marufuku shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani kinyume kabisa na matakwa ya Katiba na Sheria inayoendesha vyama vingi hapa nchini.

Kimsingi Rais Magufuli ametangaza vita dhidi ya demokrasia ya vyama vingi. Anatekeleza kikamilifu imani ya chama chake kuhusu mfumo wa vyama vingi bila kificho kama walivyofanya viongozi wenzake waliopita.

Kimuundo, CCM ni chama chenye taswira kamili ya kikomunisti. Vyama vya kikomunisti haviamini katika siasa za ushindani kama njia halali ya kupata viongozi. Vyama hivi vinaamini katika kupata viongozi kupitia kundi la viongozi wahafidhina wanaoamninika kuwa na busara kuzidi wengine.

Ni kundi hili ambalo limekuwa likitoa wagombea urais wa CCM, na vikao hutumika tu kuhalalisha uamuzi wa kundi hili la ‘wazee wenye busara’. Ndiyo maana uenyekiti wa CCM ni wa kupishana pamoja na kwamba Katiba yao inasema kwamba atachaguliwa na Mkutano Mkuu.

Bahati mbaya mfumo wa kupata viongozi ndani ya CCM umeambukiza hata vyama vya upinzani. Pamoja na kwamba vyama vya upinzani vinahubiri demokrasia lakini haviamini katika utashi wa wanachama wao kuchagua viongozi wanaowataka.

Kama ilivyo kwa CCM, vyama vyama vingi vya upinzani vimetengeneza mazingira ya kuhakikisha kwamba wateule fulani ndiyo wanaopewa nafasi za uongozi. Uchaguzi na uteuzi wa viongozi wakuu wa vyama vyote vikongwe vya upinzani hufanyika kikomunisti kama ilivyo kwa CCM.

Kundi la watu wachache wahafidhina hukaa na kuamua nani awe kiongozi na vikao vya chama hutumika tu kuhalalisha matakwa ya kundi la wateule. Hali hii kwa kiasi kikubwa imeufanya mfumo wetu wa siasa uendelee kuwa mfumo wa chama kimoja wenye matawi mengi!

Sasa ujasiri wa Rais Magufuli wa kukataa kuishi na vyama vya upinzani kinafiki kama walivofanya wenzake una faida na hasara zake. Kwanza, ni vigumu mno kwa kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia akafanikiwa kutawala kidikteta.

Ukiwa zao la kidemokrasia utafanikiwa kutawala kama utatawala kidemokrasia. Ukitaka kutawala kidikteta hakikisha unaingia madarakani kwa njia za kidikteta. Kiongozi aliyeingia madarakani akataka kutawala kidikteta atataseka mno na atajikuta anapoteza muda mwingi wa kufanya shughuli za maendeleo katika kuhangaika na wapinzani na makundi mengine ya kupigania haki za kiraia.

Pili, kuna tafiti za kutosha zinazoonyesha uhusiano uliopo kati ya demokrasia na maendeleo. Kwa ujumla, tafiti zinaonyesha kwamba demokrasia na maendeleo ni sehemu mbili za sarufu moja.

Ndiyo kusema huwezi kupondaponda upande wa demokrasia bila kuumiza upande wa maendeleo. Nchi nyingi zilizoendelea na zinaendelea kwa kasi ni zile ambazo zimekumbatia demokrasia. Hakuna utafiti wowote unaoonyesha hasara au ukinzani wa demokrasia dhidi ya maendeleo ya binadamu

Tatu, katika ziara zake barani Afrika Rais Obama amekuwa akiwaasa viongozi wa Afrika kuzingatia mambo mawili kama wanataka nchi zao ziendelee kuwa rafiki wa Marekani na nchi za magharibi kwa ujumla.

Mambo haya ni kuruhusu uhuru wa habari na uwepo wa vyama vingi na kuvipa vyama vya upinzani nafasi ya kufanya shughuli zake bila bughudha. Mambo yote haya mawili inaoenekana Rais Magufuli amepania kuyaondoa tena mapema iwezekanavyo katika utawala wake.

Sasa hasara moja ni kwamba utawala wa Rais Magufuli una hatari ya kuingiza nchi katika mgogoro mkubwa na Marekani na mataifa mengine ya magharibi. Hili likitokea hatutakuwa salama kama nchi.

Hakuna nchi yoyote maskini inayoweza kuwa salama kwa kugombana na Marekani na mataifa mengine ya magharibi. Mifano ipo mingi lakini kwa karibu kabisa tunaweza kujikumbusha ya Zimbabwe.

Kwa hiyo Rais Magufuli ana hiari ya kuchagua jambo moja kati ya mawili kuhusu atakavyotawala ndani mfumo wa vyama vingi. Mosi, Rais Magufuli anaweza kuchagua kuendelea kuchapa kazi na kutekeleza ilani ya chama chake na ahadi zake huku akiwa na ujasiri wa kuviacha na kuvipa nafasi vyama vya upinzani vifanye kazi zake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

Kwa kufuata mkondo huu mimi naamini atafanikiwa sana na ifikapo mwaka 2020 atashinda kwa kishindo cha kutisha.

Pili, Rais Magufuli anaweza akavaa ujasiri wa kuachana na unafiki wa viongozi waliomtangulia wa kuruhusu mfumo wa vyama vingi kwa shingo upande. Hii inaamanisha kwamba ataendelea na juhudi alizozianza hivi karibuni za kuzuia vyama vya siasa kufanya shughuli na yeye pekee kubaki kuwa mwanasiasa katika nchi hii, na hatimaye kudhoofisha na hata kuuangamiza kabisa mfumo wa vyama vingi nchini.

Akifanya hivi atakuwa ameiingiza nchi yetu rasmi katika utawala wa kidiktea na atakuwa ametangaza vita kubwa dhidi ya demokrasia. Ujasiri huu ndio utakuwa udhaifu wake na pengine anguko lake kisiasa na kiuongozi. Kama ambavyo yeye mwenyewe ametusihi mara nyingi, tumuombee kwa Mungu asifike huko!
Source:Raia Mwema.
 
huyu mtu anaongeaga ukweli jaman. hakuna democrasia kwenye vyama, au niseme tu hakuna democrasia Africa.
 
Namkubali sana Kitila Mkumbo katika maandishi yake, nalikumbuka sana andiko lake la Mwaka jana kua wapinzani waliozoea siasa za matukio zimepitwa na wakati.. Wafanye siasa za masuala.

Pia nimependa alivyotoa ushauri kwa JPM.. na Nchi.. Pia nimemuelewa alivyozungumzia ufinyu wa Demokrasia ndani ya vyama vya upinzani, ili kwangu ni kubwa sana kwa wapinzani.. Nilitarajiwa vyama vya upinzani visiwe na makando kando yoyote Yale.. Lakini nitoafauti kabisa, vinaendeshwa kwa ujanja ujanja tu.

Ila nakataa mfano wa demokrasia kwa Zimbabwe, kua ndio uliosababishwa kuwekewa mbinyo, hii nakataa.. Ishu ya kunyang'anywa mashamba kwa wazungu.. Ndio iliosababishwa wafikie pale.. Maana ukiangalia Zimbabwe kulikua na serikali ya mseto, Uganda ambapo upinzani upewi nafasi yoyote, wanabuguziwa kuliko kawaida hawana vikwazo alafu Zimbabwe kuliko kua na serikali ya mseto Kuna vikwazo
 
Mwenyewe siamini kwenye hii kitu inayoitwa demokrasia kama inafanya kazi Africa, Demokrasia maana yake ni maoni ya wengi, na Afrika wengi ni wajinga, hawana exposure kuhusu mambo ya utawala na wajibu wa viongozi wao viongozi wao, hivyo demokrasia Africa inaturudisha nyuma zaidi kuliko mbele
 
Mkumbo anaongea point.
Point ya Mkumbo hapo ngoja nijaribu kuinukuru ni kuwa Magufuli awaache kinafiki nafiki wapinzania kwa sababu hata demokrasia wanayolilia sio demokrasia bali ni unafiki. Kwa hiyo Magufuli asihangaike na wanafiki
 
Message Delivered Proff... Nimeanza kuelewa yale yanayosemwa toka kuondoka KWAKO.... jamaa wa UFIPA wamepoteza DIRA ....Ulikuwa hazina kubwa sana.... Kwa ukweli hawa jamaa wamekuwa sio wenyewe TENA hadi tunashangaa ni nini KIMEWAKUMBA!!!
 
Mwenyewe siamini kwenye hii kitu inayoitwa demokrasia kama inafanya kazi Africa, Demokrasia maana yake ni maoni ya wengi, na Afrika wengi ni wajinga, hawana exposure kuhusu mambo ya utawala na wajibu wa viongozi wao viongozi wao, hivyo demokrasia Africa inaturudisha nyuma zaidi kuliko mbele

....exactly; ukienda vijijini uwaulize demokrasia ni nini hawawezi kukujibu!, na huko ndiko ccm huwa wanashinda kwa kishindo kila mwaka!, safari bado ndefu sana.
 
Kwahiyo chama chake chenye kiongozi mkuu ndio chenye demokrasia?
 
Eti unamkubali sana Kitila Mkumbo, kumbe unakubali yale uyatakayo wewe na mengine usiyoyataka hukubaliani nayo!!! Acha unafiki wa kumkubali mtu nusu nusu halafu kudai eti unamkubali sana.

Back
Top Bottom