Kitengo maalum cha kudhibiti ajali za barabarani kianzishwe

amanimaendeleo

JF-Expert Member
Oct 29, 2015
251
75
KUTOKANA NA AJALI ZA BARABARANI KILA SIKU KUTOKEA NA KUSABABISHA AJALI ZENYE KULETA MAAFA KWA WATU NA ULEMAVU IMEFIKA WAKATI KIANZISHWE KITENGO MAALUMU KIWEZESHWE KIWEZE KUSIMAMIA MATUMIZI SALAMA YA BARABARA NA KUSIMAMIA KIKAMILIFU SHERIA ZA BARABARA.
VILEVILE MADEREVA WOTE WA MABASI NA MALORI WAFANYIWE UHAKIKI MAALUMU KUJUA KAMA WANASTAHIKI KUENDESHA MAGARI ,LESENI ZAO WALIPATA KIHALALI AU ISIVYO KIHALALI NA WAFANYIWE UKAGUZI KILA WAKATI.
KITENGO CHA KUTOA LESENI ZA UDEREVA KIDHIBITIWE KIFANYE KAZI YAKE KISHERIA PASIPO UDANGANYIFU.
KUWEPO NA PATROL ZA WAKAGUZI BARABARA ZOTE SIO SEHEMU MAALUMU TU.
MFANO DEREVA ANASABABISHA AJALI ANAKIMBIA HAPATIKANI, KUDHIBITI HII HALI MADEREVA WOTE WANAPEWA KAZI BAADA YA KUWA NA WADHAMINI WA UHAKIKA 3 WENYE MALI ZISIZOHAMISHIKA.
TUSIRAHISISHE MAMBO HII TABIA NDIO INALETA MADHARA KILA SIKU.
KITENGO CHA USALAMA BARABARANI KWA SASA NAONA KAMA KIMEZIDIWA KABISA
UWEKEZAJI WA KUTOSHA UFANYIKE KUDHIBITI HAWA MADEREVA WAHUNI WANAOSABABISHA AJALI MAKUSUDI AMA SIVYO HALI ITAZIDI KUWA MBAYA
 
Back
Top Bottom