Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,590
- 28,761
Jema shada la maua, laua kwa rangi yake.
Limepambwa kwa murua, sioni kifani chake.
Na asumini kutiwa, hakika mahala pake.
Shada hili limea, na pepo na watu wake.
♥
Haya maua thamini, waku2nukiwa nan?.
Rehani na mawaridi, hizo ndizo shanga zake.
Tena halafu mkadi, limefungwa yasitoke.
Harufu yake baridi, shada hli sifa yake.
Shada hili zuri hali, mstadi fundi wake.
Kachori linaponukia, utasema zumaridi.
Jinsi linavyonukia, kwa uzuri limezidi. Hadi limetimilia, shada hili ni shadidi.
Nami nalitunikia, sifa yake maridadi.
♥
Shada kiwekwa shingoni, hupendeza sawasawa.
Huvutia kwa makini, kama sahani na kawa.
Huvutia mashetani, na majini wenye mbawa.
Malaika na rukhani wote wanalitambua.
♥ SHADA HILI SHADA GANI, wanaMMU NAMBIENI. HAYA MAUA THAMINI WAKUTUNUKIWA NANI.......? ♥