Kitendawili cha Wamakonde wa Kipumbwi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,253
KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU: KITABU KIONGOZI KATIKA VITABU VYA HISTORIA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Nakumbuka mara ya kwanza nilipoonana na Dr. Harith Ghassany nyumbani kwake Muscat aliyenipeleka alikuwa Abdullah Amour ambae sasa ni marehemu na alikuja kuwa rafiki ndugu na alikuja hadi Tanga kunitembelea.

Ilikuwa mwaka wa 1999 ndipo nilipokutana na Dr. Harith Ghassany.

Mwezi wa Ramadhani ulinukuta Muscat Harith alinialika futari nyumbani kwake.

Harith alinifahamisha kuwa ana azma ya kuandika kitabu kuhusu Zanzibar na hapo ndipo nilipomfahamisha kisa nilichosikia Tanga kuwa kulikuwa na kambi ya Wamakonde Kipumbwi ambapo ndipo walipokuwa hawa Wamakonde wakipewa mafunzo kisha kuvushwa kwenda Zanzibar kuipigia kura ASP uchaguzi wa wa 1961 na mwaka wa 1964 kushiriki katika mapinduzi.

Harith alinisikiliza kimya wala hakunisaili na akasema kuwa atakuja Tanga ambako mimi ndiko nilikokuwa naishi.

Alifika Tanga na nikaweka miadi na Mzee Mohamed Mkwawa.

Nilimshusha Harith nyumbani kwa Mzee Mkwawa sehemu za Kisosora kisha mimi nikaendelea na shughuli zangu nyingine.

Niliporudi mchana kumchukua kitu kilichonistaajabisha ni kuwa nilimkuta Harith kakalia mgongo, kachoka na kasawajika.

Sikusema neno.
Tulikuwa tumeandaliwa chakula cha mchana.

Nakumbuka tulipiga kipunga na samaki.
Kumaliza namwambia Harith twende zetu.

Jibu alilonipa lilinishangaza.

''Guy wewe nenda njoo nichukue jioni mimi na Mzee Mkwawa hatujamaliza mazungumzo yetu.''

(Mimi na Harith tunaitana, ''Guy,'' na hiki ni kisa naamini mtapenda kukisikia tulihadithiwa na Mzee Ahmed Rashad mkasa wake na rafiki yake Ahmed Abdullah Alkharui maarufu kwa jina la Bamanga.

''Guy,'' ndilo jina wakiitana.

Marafiki hawa mwaka wa 1952 walishitakiwa mahakamani kwa kosa la uchochezi).

Nikashangaa nikajiambia haya mazungumzo toka asubuhi hadi dhuhri yapata saa nne hayajesha na sasa wanaendele ahadi alasiri...

Nilipokuja kumchukua jioni ile alipoingia kwenye gari kitu cha kwanza nilichomuuliza ilikuwa, ''Guy imekuwaje mbona umechoka hivyo umenitisha sana leo.''

''Sikiliza Guy, ufunguo wa kitabu chetu anao Mzee Mkwawa mimi nimetembea maktaba zote kubwa sijakuta haya aliyonieleza Mzee Mkwawa.''

Kwa mara ya kwanza Harith anaelezwa na Mzee Mkwawa yaliyotokea Pemba ya yeye kushauriwa akimbie Pemba asije kuuliwa na Hizbu.

Mkwawa wakati huo kijana labda wa miaka 25 alikuwa mwanachama wa ASP na mmoja wa vijana wa kazi wa Abeid Amani Karume.

Alipofika Tanga akadakwa na Ali Mwinyi Tambwe na wenzake na kumuomba msaada wa yeye kurejea Zanzibar kwa kazi maalum ya ''kufa na kupona,'' kwa ajili ya uhuru wa Waafrika wa Zanzibar.

Mimi sasa nikawa nayasikia hayo mengine kwa mara ya kwanza kutoka kwa Harith.

Mzee Mkwawa kumbe hakunipa yote.
Nilishusha pumzi.

Sikushangaa kwa nini Harith nilimkuta kakalia mgongo wake na kachoka sana.

Hakika Mzee Mkwawa alikuwa kashika ufunguo wa kitabu chake Dr. Harith Ghassany.

Kilichobaki ilikuwa kumfikisha Dr. Harith Ghassany Kipumbwi kisha amkutanishe na Victor Mkello.

Ali Mwinyi Tambwe ana historia ya pekee katika historia ya Tanganyika na Zanzibar na leo hakuna anaeijua historia yake.

Kuna picha katika kitabu cha Abdul Sykes inauonyesha Ali Mwinyi Tambwe amekaa pembeni kwa Kleist Sykes na Abdul Sykes yupo katika picha hiyo mtoto mdogo wa shule ya msingi.

Hii ni picha ya mwaka wa wa 1936 ya viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Mwaka 1953 huyu Ali Mwinyi Tambwe alikuwapo nyumbani kwa Hamza Mwapachu katika mazungumzo kati ya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu walipojadili na kukubaliana kumtia Julius Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA na 1954 waunde TANU.

Huyu Ali Mwinyi Tambwe ndiye aliyemtia Mohamed Mohamed Omar Mkwawa katika vyombo vya usalama na kumpa usimamizi wa kambi ya Kipumbwi.

Inasemekana Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mtu wa Special Branch toka ukoloni.

Hii ndiyo barabara Mzee Mkwawa aliyompitisha Dr. Harith Ghassany hadi kumfikisha Kipumbwi kisha akampeleka Nguvumali Tanga mjini nyumbani kwa Victor Mkello.

Watafiti wote wa historia ya mapinduzi hawakuwajua watu wa mfano wa Mzee Mkwawa kwa hiyo walipitwa na sehemu muhimu sana katika historia ya Zanzibar.

Kichekesho kikubwa ni kuwa na hata wale waliowajua Wapinduzi hawa wanajifanya kama vile watu hawa hawakupata kuwepo.

Wamejifanya pia hawajui kuwa Victor Mkello alikutana na Mzee Karume Zanzibar baada ya mapinduzi na Mzee Karume alimshukuru kwa kazi yake.

Picha ya kwanza Dr. Harith Ghassany na Mzee Mohamed Omari Mkwawa Tanga.

Mimi binafsi namshukuru sana Dr. Harith Ghassany kwa kunishirikisha katika utafiti wake na huu utafiti ndiyo ulionifunza hstoria ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Picha ya pili nyumbani kwa marehemu Mzee Ahmed Rashad Ali, Upanga Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kushoto Ahmed Rashad, Dr. Harith Ghassany na Mohamed Said.

Picha ya tatu nikiwa nyumbani kwa Dr. Harith Ghassany Muscat mwaka wa 2015.

Screenshot_20211115-210953_Facebook.jpg
 
Sheikh Mohamed,

Masimulizi ya hawa watu wawili, yaani Mohamed Omar Mkwawa na Victor Mkello hayapo popote katika vitabu rasmi vya historia ya mapinduzi ya Zanzibar

Je hii ni bahati mbaya, sahau, au pengine waandishi wa historia hiyo kuona kipande cha ushiriki wao hakikua “significant?”
 
Sheikh Mohamed,

Masimulizi ya hawa watu wawili, yaani Mohamed Omar Mkwawa na Victor Mkello hayapo popote katika vitabu rasmi vya historia ya mapinduzi ya Zanzibar

Je hii ni bahati mbaya, sahau, au pengine waandishi wa historia hiyo kuona kipande cha ushiriki wao hakikua “significant?”
Sesten...
Hii ilikuwa siri kubwa.

Kwanza Wamakonde wamevushwa kuvamia nchi huru wakitokea Tanganyika.

Pili hawa Wamakonde waliua Waarabu wengi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom