Kitendawili cha ndoa.

Kitendawili cha ndoa.

Daniel Adrian

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
311
Reaction score
335
Hapa nipo nje ya nyumba ya ibada baada ya ibada ya siku leo. Kwa mbali kidogo naskia watu wazima (50 -60 yrs ) wanazungumza. Wanazungumza kuhusu ndoa, wanasema "ndoa ni pasua kichwa", ndoa ni ngumu kushughulika nayo, "ndoa inahitaji uvumilivu wa chuma".

Kiukweli sio mara moja kusikia watu walio kwenye ndoa wakilalamika hivyo na hali hii imekuwa ya kawaida lakini kinachonitisha ni kuwa why malalamiko ya ndoa ni mengi sana ?
Jambo hilo linachanganga sana. Na wakati mwingine linafanya mtu asielewe changamoto ziko wapi maana mi nnachojua " mapenzi ni matamu", na kuishi na mtu umpendae ni raha.

Sasa mie bado sijaingia katika ndoa hivyo nimeona hili linanihusu sana maana nna mpango wa kuoa.
Sasa nimeona hii ni mada moto sana. Nimeileta kwako ili ipata deserved discussion kwamba kwanini ndoa inasemekana kuwa changamoto sana ?

Watu wazima, na ambao mmekuwa kwenye ndoa hebu tusaidieni, ugumu wa ndoa uko wapi hasa ? Tukiachana na changamoto za kifedha na huduma.
 
Kwani watu wazima hawana kasoro ?

Kwani vichaa hawawezi kuzeeka na kufikia umri wa miaka60

Kama unajiona una umri na uwezo wa kuingia kwenye ndoa ingia uje kuwa mfano kwa watu wengine..

Hizo story za watu wazima sio kila kitu unachokiskia kwako ukichukie kama kilivyo,jiongeze
 
Mtu anaingia kwen ye ndoa ndoa baada ya kuziweza changamoto suruba za kuishi peke yake hivyo anatafuta changamoto zingine azihimili vyema baada ya hapo anatafuta kuzaa watoto kuongeza changamoto na kuzitatua fresh . Ukimuona analalamika na ndoa jua hakuweza Kuzihimili changamoto za kuishi pekee yake atawezaje kuhimili changamoto za kuishi na MTU mwingine?

Unapotaka kuoa au kuolewa jitathimin jinsi unavohimili changamoto je ukiwa na mwingine itakuwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usifikirie UZINIFU,,,ridhika na ULIYE NAE,, ridhika na MAISHA YAKO....mpende ULIYE NAE...HIYO NDY SIRI YA NDOA.,,watu wengi NDOA ZINAWASHINDA sababu HAWARIDHIKI NA MKE/MUME WALIE NAE, ,,pia bado ni WAZINIFU....yupo kwnye NDOA,,LAKINI ana mahusiano na WATU 6 NJE...na wote anawapenda zaidi ya MUME/MKE wake aliye NAE ndn ...unadhani utaacha kuona NDOA NGUMU?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom