Kitabu cha mapenzi kati ya Myahudi na Mpalestina chauza

Quickly

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,056
649
Kitabu cha mapenzi kati ya Myahudi na Mpalestina chauza

9 Januari 2016
160109143841_dorit_640x360_bbc_nocredit.jpg

Kitabu cha mapenzi kati ya raia Myahudi na mwenzake Muislamu wa Palestina kinaongoza kwa mauzo baada ya wizara ya elimu nchini Israel kukataa kukiorodhesha katika mtaala wa elimu shuleni.
Maafisa walihofia kwamba Borderlife kilichotungwa na Dorit Rabinyan kinaweza kuongeza uhusiano wa kimapenzi kati ya raia wa Kiyahudi na wenzao wa Kiarabu.
Lakini hatua hiyo ilizua hisia kali na kukifanya kitabu hicho kununuliwa na wengi.
Uchapishaji ughaibuni pia unaharakishwa na tafsiri yake inajadiliwa nchini Hungury,Uhispania na Brazil.
Ajenti wa Bi Rabinyan amesema kuwa zaidi ya vitabu 5,000 vimeuzwa katika juma moja pekee,vingi vikiuzwa katika soko la Israel huku maduka mengi yakiwa yamemaliza vitabu hivyo.

Kitabu cha mapenzi kati ya Myahudi na Mpalestina chauza - BBC Swahili
 
So, what's the issue here? Kwani mapenzi ni kitu cha ajabu?
 
hawa watu kwa kupiga deal tu ndiyo wenyewe...ma fake life kila siku kwa ajili ya biashara, anyway, tuwaige kuliko kulalamika!
 
Kwahiyo Wamefunga Ndoa Kabisa Au Wanapeana Raha Tu. Lakin Hapo Wasiopenda Hayo Mausiano Zaid Ni Waisrael Watakufa Na Chuki Zao. Dada Yao Kaishazimika Kwa Mwarabu, Taqarab Taqarab Ya Habib, Habib Yanur Lahin
 
Kumbe ni hivyo tu! Na mimi ngoja nije nichapishe cha kwangu na mpenzi wangu "Swarhh'na" sijui inaandikwa hivyo? Naomba jamaa zangu wa upande wa pili mnisaidie!
 
Back
Top Bottom