Kiswahili ni Lugha yetu, tuitumie vyema

Safari Safi

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
2,697
2,000
Ili mawasiliano katika lugha yawe ssahihi lazima tulinde, ama tujali maana za maneno,

Mifano:
Neno "Hatakua" au"Hatakwenda"
mtu anatumia "atakuwa" au "atakwenda"

maneno hayo, ukiyatumia kwa rafudhi hizo za "kihaya" unabadilisha maana kuwa kinyume chake. (yasome upya uone)

maneno mengine ukiyatumia ki makosa yanapoteza maana kabisa,

Mfano
"Ela" badala ya "Hela" ela ni kitugani?
"Esabu" badala ya "Hesabu" tafakari, nipe maana ya esabu mi sielewi, kama maneno hayo yana maana katika lugha ya kiswahili ni miongoni mwa maneno yasiyotumiwa mara kwa mara na jamii kwa hiyo si tu kwamba hayaeleweki, ila hayaleti maana halisi pia.

Kwetu tunaoshinda mitandaoni kuadika vitu vinavyosomwa na watu dunia nzima kuna haja ya kujiongezea maarifa ya lugha tunayotumia, Hasa ukizingatia kwamba sisi (watanzania) ni waasisi wa Kiswahili Duniani.

Pia ni vyema kujua, maneno yanapotamkwa kwa uvivu
huleta tofauti ya maana
mfano:

Maradhi, Magonjwa wakati Marazi ni vifaa vya kutumia ulalapo, kitanda,godoro,shuka,neti mto, kwa pamoja, ila maneno hayo hutumiwa kinyume.

kuna tofauti kati ya "Kalamu" na "Karamu"
unapotamka "karamu" maana yake, Tafrija, sherehe. na kalamu ni ya kuandikia,
kwa hiyo unapotamka neno kinyume kwa herufi moja tu! linaleta maana kinyume, kwa mujibu wa mfano huo.

Pia kuna tofauti ya "kushika" na "kukamata",

kuna tofauti kati ya "kusimama" na "kuinuka"

mtu alikuwa kainama, halafu umemwona yuko wima, unapaswa kusema kainuka, siyo kasimama!

akiwa amekaa usiseme "inuka" hajainama, sema "simama"
kama alikuwa anakimbia, kisha ukamuona wima maana yake kasimama,

kuna tofauti kati ya "kooni" na "shingoni"

kuna tofauti kati ya "kuswali" na "kusali"

kuna tofauti kati ya "Hotel" na "Hostel"

kuna tofauti kati ya "kura" na "kula"
kura = kwenye uchaguzi, na "kula"Chakula

kuna tofauti kati ya "samani" na "thamani"
samani = vyombo vya nyumbani kabati meza sahani vikombe vitanda vyote kwa pamoja vinaitwa "samani"

thamani ni "Value" mfano
Dola moja ya marekani ni sawa na thamani ya sh 2180 za Tanzania.

wapo wataalamu humu ndani, wataendelea kutukumbusha!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom