Yote ni sahihi na kutegemea orientation na audience, muandishi anaweza kuchanganya. Haya maneno yanatokana na lahaja tofauti za Kiswahili, ndiyo maana wengine husema hapo na wengine husema papo, na wengine huchanganya na kusema papo hapo (Kiswahili cha biblia kime influence sana hii style ya kuchanganya lahaja kwa sababu audience yake ilikuwa wanaoongea Kiswahili wote na lahaja zote kubwa).
Wengine watasema anaoga, wengine watasema anakoga, wengine watasema anaenda, wengine watasema anakwenda, yote maneno ya Kiswahili sawia, tofauti lahaja tu.
Hebu kwanza tuanze kunyumbua maneno ndipo tutaona neno gani ni sahihi.
Mzizi wa neno ONYESHA ni ONY-A ambapo ukiunganisha unapata kiini cha neno ambacho ni ONYA
Vivyo hivyo ONESHA ni ON-A =ONA
Turudi kwenye mfano wa sentensi hizo mbili
Sentensi sahihi ni CHADEMA YAONESHA DEMOKRASIA.
ina maana demokrasia inaonekana sio inaonyesha. ONYESHA inatokana na neno ONYA ambalo kwa tafsiri yake ni kama mtu ukikosea jambo fulani pale UNAONYWA.
Wataalamu wa Kiswahili hebu changieni mawazo yenu hapa.