Kiswahili kitunzwe, kienziwe – Waziri Mbarouk

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
DSC09953.JPG

Mwashungi Tahir na Zuleikha Abdulla (ZJMMC)

WAZANZIBARI wametakiwa kuitukuza lugha ya taifa lao ili kuimarisha maendeleo ya haraka nchini kama ilivyo kwa nchi nyengine.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk, alisema hayo katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani mjini hapa, alipokuwa akizindua Baraza jipya la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA).


Alisema lugha ya kiswahili ni lugha iliyozoeleka kwa wazanzibar, hivyo hakuna budi kuiendeleza na kuitumia katika matumizi ya kila siku.


Alifahamisha kuwa wakati umefika sasa kwa wazanzibari kuipa hadhi lugha yao na kuitumia katika shughuli mbalimbali hasa za kitaifa.


"Kutumia lugha za kigeni katika shughuli muhimu kama vile semina na kongamano ni sawa na kuishushia hadhi lugha ya kiswahili, hivyo ni lazima kuipa hadhi lugha hiyo na itumike kwa shughuli mbalimbali.


Aidha alisema lugha ya kiswahili imekuwa ikitumika katika mikutano ya kimataifa, jambo ambalo linaonesha dhahir lugha hiyo kutambulikana ulimwenguni.


"Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha lugha ya kiswahili inatumika ipasavyo kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo,"alisema.


Sambamba na hilo, lakini Waziri huyo, aliahidi kushirikiana na watendaji wa baraza hilo, kwa lengo la kuikuza na kuendeleza istilahi za lugha ya kiswahili.


Nae Mwenyekiti wa Baraza hilo, Amour Abdullah Khamis, aliwashukuru wajumbe wote waliomaliza muda wao kwa kushirikiana katika kipindi chote cha kazi.


"Changamoto kuu ya baraza letu ni kufanya kazi kwa uzalendo na kushirikiana ili kufikia malengo tuliojiwekea ,"alisema.


Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Khadija Bakari, alisema jukumu la baraza ni kukilinda, kukihifadhi na kukiendeleza kiswahili ndani na nje ya Zanzibar.


BAKIZA imewezesha lugha ya kiswahili kutumika hadi nje ya nchi kupitia katika vyombo vya habari kama vile BBC, Radio ya Kimataifa ya China, Sauti ya Ujerumani na Moscow, Baraza hilo lina wajumbe 16.










Imewekwa na MAPARA at 1:01 PM
 
Back
Top Bottom