Ijumaa ni wikendi kwa waarabu, Jumamosi wikendi kwa wayahudi na Jumapili ni wikendi kwa wakristo na nchi za magharibi. Juma linaanza Jumatatu kwa utaratibu kwa nchi za magharibi. Kumbe juma linakwisha Jumapili (wikendi)
Sisi waswahili tumezipa siku majina kwa kufuata utaratibu wa Kiarabu ambao juma huisha Ijumaa. Kumbe Jumamosi ni siku ya kwanza ya juma. Ndiyo maana inaitwa na waswahili Juma-mosi, yaani siku ya kwanza ya juma.
Kumbe kwa majina ya siku tumefuata utaratibu wa Kiarabu, lakini kwa kupanga juma tumefuata utaratibu wa Kimagharibi ambapo juma huanza Jumatatu na kuisha Jumapili.