KISUTU, DAR: Kesi namba 456 yaahirishwa hadi kesho; Hakimu asisitiza anataka iishe Ijumaa hii!

KISUTU, DAR: Kesi namba 456 yaahirishwa hadi kesho; Hakimu asisitiza anataka iishe Ijumaa hii!

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Kesi hii ipo chini ya Hakimu Simba ambaye ameanza kwa kusema:

“Ninataka kesi yangu imalizike.

Tupange kesho (Desemba 21, 2017) tukutane saa tano, Upande wa Jamhuri hakikisha mnaleta mashahidi wote. Nataka hadi kufika Ijumaa kesi yetu iwe imekwisha. Kama itakwenda kwenye defence iende. Kuahirisha kesi kwenda hadi mwaka ujao kuna shida. Tusipojipanga tutatoka saa nne usiku.”

Wakili wa Jamhuri aliyekuwepo ni Batilda Mushi ambaye alikuja na shahidi. Wakili wa Utetezi alikuwepo Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya.

Kesi imeahirishwa hadi kesho saa tano kamili asubuhi.

Kujua tulikotokea, soma > Kesi namba 457 (Jamhuri vs JamiiForums): Shahidi wa nne atoa ushahidi, kielelezo chake chazua mjadala
 
Hamna kesi hapo, ni usumbufu wa hovyo sana.

Ndio maana Hakimu ameamua kukomaa iishe tu
 
Hakimu anajua hamna kesi hapo..
Ndio maana anaona hakuna haja ya hili shauri kupelekwa hadi mwakani.
 
Hayo maneno ni ishara ya ushindi kwa JF!

Ndiyo maana hata hakimu "kacoñclude" anataka iishe haraka!
 
Hakimu keshaandaa hukumu. Anachongojea ni formality. Mwisho wa siku mtamsikia hakimu akisema, 'Hakuna ushahidi wa kutosha kumtia mtuhumiwa hatiani'. Case dismissed...
 
Back
Top Bottom