VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
[FONT=trebuchet
ms]Sababu hasa ya dana dana za jana za kufuta mashtaka na
kuyafungua tena dhidi ya Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA sasa zi wazi.
Chanzo cha kuaminika kinasema kuwa kiukweli dana dana za jana zilifanywa
ili kumuondoa Mheshimiwa Hakimu Mkazi,Emilius Mchauru.
Chanzo hicho kimedai kuwa 'Wazee' wa Usalama walitumwa 'kuchungulia'
uamuzi wa Mheshimiwa Mchauru na kuona kuwa Mheshimiwa huyo alijiandaa
kusoma uamuzi wake ambao ungewapa dhamana washtakiwa wote:Alfred
Muganyizi Lwakatare na Ludovick Joseph Rwezaura kwa kutumia kesi maarufu
ya jinai ya Daudi Pete dhidi ya Jamhuri( Mahakama ya
Rufani ilijulikana kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya
Daudi Pete).
Katika kesi hiyo,Daudi Pete alishtakiwa Mahakama ya Wilaya kwa ujambazi
ambapo alinyimwa dhamana kwa kutumia kifungu cha 148(5)(e) cha Sheria ya
Mwenendo wa Makosa ya Jinai,1985 kilichokuwa kinakataza dhamana kwa
makosa ya ujambazi. Baadaye,Daudi Pete alikata rufaa Mahakama Kuu
kupinga kunyimwa dhamana. Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Hayati Jaji
Mwalusanya ilimpa dhamana Daudi Pete na kutamka kuwa kifungu hicho kiko
kinyume na Katika kwakuwa kinapingana na Ibara ya 15(2) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977.
Ikumbukwe kuwa tangu Jumatatu,Mawakili wa Serikali walisema kuwa
mashataka ya ugaidi hayana dhamana.Hii ni kwakuwa kifungu cha 49 cha
Sheria ya Kuzuia Ugaidi,2002 kinakataza dhamana kwa makosa yahusuyo
ugaidi. Kifungu hiki cha 49 cha Sheria hii kimerekebisha kifungu cha 148
cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai,1985 kilichozungumzwa katika
kesi ya Daudi Pete.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu na
kukata rufaa Mahakama ya Rufani. Hapo,jopo likiundwa na Hayati Jaji Mkuu
wa zamani Francis Nyalali,Jaji Lewis Makame na Jaji (baadaye Jaji Mkuu
mstaafu) Agustino Ramadhani,lilikubalina na maamuzi ya Jaji Mwalusanya
na hivyo Serikali kupigwa mweleka. Tangu hapo,Mahakama ya Rufani
ilitamka na kuamuru kuwa dhamana zitatolewa kimahakama hata kama sheria
itakuwa inakataza.
Hivyobasi,jana washtakiwa wangeachiwa kwa dhamana kama si Mkurugenzi wa
Mashtaka kufuta na kuanzisha upya kesi ya akina Lwakatare. Kufuta kuna
maana kuwa kesi hiyo imeanza upya ingawa mashtaka yote ni yale yale na
Mahakama ni ile ile. Amebadilishwa Hakimu tu.Sasa ni Mheshimiwa Hakimu
Mkazi Aloyce Mtekama.
Chanzo hicho kutoka kwa DPP kinadai kuwa tangu Jumatatu,Hakimu Mchauru
aliwaudhi 'wakubwa' kwa kuwataka washtakiwa kukubali au kukana mashtaka
dhidi yao. Kesi iliyofutwa ni Nambari 37 ya 2013 na mpya ni Nambari 6 ya
mwaka 2013. Haihitaji weledi sana wa kisheria kujua hapa pia kuna
kichekesho. Iweje iliyofutwa iwe 37 halafu mpya iwe 6? Ipi ilianza?
' Hakimu Mchauru ameonekana hafai. Hakimu Mtemana atakuwa na kazi ngumu
sana.Lazima awe makini na kesi hii inayogusa maslahi ya wakubwa.'
kilimaliza chanzo hicho
VUTA-NKUVUTE
aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam[/FONT]
Sababu hasa ya dana dana za jana za kufuta mashtaka na kuyafungua tena dhidi ya Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA sasa zi wazi. Chanzo cha kuaminika kinasema kuwa kiukweli dana dana za jana zilifanywa ili kumuondoa Mheshimiwa Hakimu Mkazi,Emilius Mchauru.
Chanzo hicho kimedai kuwa 'Wazee' wa Usalama walitumwa 'kuchungulia' uamuzi wa Mheshimiwa Mchauru na kuona kuwa Mheshimiwa huyo alijiandaa kusoma uamuzi wake ambao ungewapa dhamana washtakiwa wote:Alfred Muganyizi Lwakatare na Ludovick Joseph Rwezaura kwa kutumia kesi maarufu ya jinai ya Daudi Pete dhidi ya Jamhuri( Mahakama ya Rufani ilijulikana kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Daudi Pete).
Katika kesi hiyo,Daudi Pete alishtakiwa Mahakama ya Wilaya kwa ujambazi ambapo alinyimwa dhamana kwa kutumia kifungu cha 148(5)(e) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai,1985 kilichokuwa kinakataza dhamana kwa makosa ya ujambazi. Baadaye,Daudi Pete alikata rufaa Mahakama Kuu kupinga kunyimwa dhamana. Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Hayati Jaji Mwalusanya ilimpa dhamana Daudi Pete na kutamka kuwa kifungu hicho kiko kinyume na Katika kwakuwa kinapingana na Ibara ya 15(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977.
Ikumbukwe kuwa tangu Jumatatu,Mawakili wa Serikali walisema kuwa mashataka ya ugaidi hayana dhamana.Hii ni kwakuwa kifungu cha 49 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi,2002 kinakataza dhamana kwa makosa yahusuyo ugaidi. Kifungu hiki cha 49 cha Sheria hii kimerekebisha kifungu cha 148 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai,1985 kilichozungumzwa katika kesi ya Daudi Pete.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu na kukata rufaa Mahakama ya Rufani. Hapo,jopo likiundwa na Hayati Jaji Mkuu wa zamani Francis Nyalali,Jaji Lewis Makame na Jaji (baadaye Jaji Mkuu mstaafu) Agustino Ramadhani,lilikubalina na maamuzi ya Jaji Mwalusanya na hivyo Serikali kupigwa mweleka. Tangu hapo,Mahakama ya Rufani ilitamka na kuamuru kuwa dhamana zitatolewa kimahakama hata kama sheria itakuwa inakataza.
Hivyobasi,jana washtakiwa wangeachiwa kwa dhamana kama si Mkurugenzi wa Mashtaka kufuta na kuanzisha upya kesi ya akina Lwakatare. Kufuta kuna maana kuwa kesi hiyo imeanza upya ingawa mashtaka yote ni yale yale na Mahakama ni ile ile. Amebadilishwa Hakimu tu.Sasa ni Mheshimiwa Hakimu Mkazi Aloyce Mtekama.
Chanzo hicho kutoka kwa DPP kinadai kuwa tangu Jumatatu,Hakimu Mchauru aliwaudhi 'wakubwa' kwa kuwataka washtakiwa kukubali au kukana mashtaka dhidi yao. Kesi iliyofutwa ni Nambari 37 ya 2013 na mpya ni Nambari 6 ya mwaka 2013. Haihitaji weledi sana wa kisheria kujua hapa pia kuna kichekesho. Iweje iliyofutwa iwe 37 halafu mpya iwe 6? Ipi ilianza?
' Hakimu Mchauru ameonekana hafai. Hakimu Mtemana atakuwa na kazi ngumu sana.Lazima awe makini na kesi hii inayogusa maslahi ya wakubwa.' kilimaliza chanzo hicho
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
kwa mujibu wa mwananchi la leo kesi mpya ni PI No 6 wakati ile ya awali ni CC No 37.
Some tust their money into Swiss banks and others in their political power and connections But we will always trust the power of the Lord our God