Kisiwani Pemba hali yazidi kuchafuka: Polisi na Majeshi yazidi kumiminika

5523

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
2,258
2,381
Kufuatia tangazo la baadhi ya wakuu wa Mikoa Kisiwani Pemba la kupiga kafyu na baadae tangazo la Pemba nzima watu ifikapo saa 2 usiku wote wawe majumbani mwao asionekane mtu barabarani majeshi na polisi waliovalia kivita na magari makubwa makubwa yaliyobeba silaha za kivita kama ngao, bunduki nk. wanapita magari kwa magari wakiwa full kama tayari nchi tumeingia kwenye vita. Hali sasa si ya kawaida tena imekuwa ni hofu kila kona.

Haya magari hupita na kurudi bila ya kazi maalum katikati ya miji na mitaani.

Picha hizi ni leo kuanzia mida ya asubuhi hadi hivi ninavyoandika.
bandari mkoani.jpg

IMG-20160313-WA0004.jpg

Haya ni maeneo ya Mkoani Kisiwani Pemba baada ya kushushwa kutoka Bandari Kuu ya Mkoani Kisiwani Pemba

9611_10154719478859478_6210230942932940016_n.jpg

IMG-20160313-WA0006.jpg

IMG-20160313-WA0005.jpg
 
Kufuatia tangazo la baadhi ya wakuu wa Mikoa Kisiwani Pemba la kupiga kafyu na baadae tangazo la Pemba nzima watu ifikapo saa 2 usiku wote wawe majumbani mwao asionekane mtu barabarani majeshi na polisi waliovalia kivita na magari makubwa makubwa yaliyobeba silaha za kivita kama ngao, bunduki nk. wanapita magari kwa magari wakiwa full kama tayari nchi tumeingia kwenye vita. Hali sasa si ya kawaida tena imekuwa ni hofu kila kona.

Haya magari hupita na kurudi bila ya kazi maalum katikati ya miji na mitaani.

Picha hizi ni leo kuanzia mida ya asubuhi hadi hivi ninavyoandika.

View attachment 329397
Haya ni maeneo ya Mkoani Kisiwani Pemba baada ya kushushwa kutoka Bandari Kuu ya Mkoani Kisiwani Pemba

View attachment 329400

View attachment 329399

View attachment 329398
hivi ccm mkishawaua wapemba wote mtaongoza minazi na mikarafuu ?
 
Mimi nafikiri CCM bado hawajawafahamu wazanzibari vizuri. Kwanini iwanyime wananchi haki yao huku wakiwatumia polisi kutisha raia?

Polisi wa Tanzania nao huwa hawajitambui,wao ni wa kutumwa tu kama majini.

Ukweli utabaki kuwa Wazanzibari wengi hawaitaki na wameichoka CCM.
 
Machafuko ya zanzibar yamesababishwa na Jecha,huyo ndo wa kufatwa kwake na hayo magari na vifaru.
kinachofanyika sasa ni kupoteza kodi za walala hoi kisa Jecha.
Ingekuwa mamlaka yangu huyu jamaa ni wa kukamatwa na alipie gharama zote za uchaguzi na akishindwa
ni kifungo cha maisha.
 
hakuna mpemba atakayepiga kura wala atayehangaika na hilo kongamano lenu , uchaguzi ulishafanyika oct 25 na ccm iliangukia pua na kuchanika mdomo , dunia nzima inajua .
Wapemba wasipige ila waunguja watapiga. Kwani Zanzibar ni nchi ya wapemba? Wao si kwao Oman au?
 
Ukweli ni kwamba mwenye nchi ndio muaribu nchi...Watu wa visiwa hivi hawapendani na wanabaguana saana na kuleta tofauti zao mpaka kwenye siasa..Kwa style hii lazima muingiliwe kila kukicha... Kwani mmekoseana nini mpaka mnashindwa kusameheana mkapata umoja wenu ili mjisimamie wenyewe.. Acheni hila za visiwa.. Vunjeni hizo chuki msiisingizie siasa.. futeni roho mbaya muwe na umoja kamwe hakuna atakaye waingilia..!!

Usitokwe na POVU basi huo ni mtazamo wangu na uzoefu kidogo toka kwenu!!!!
 
Back
Top Bottom