Kisiasa, mwaka 2017 CCM imeimarika sana!

Ni imeimarika sana ila ili tujiridhishe zaidi hebu fanyeni kuondoa vikwazo mikutano ya kisiasa kama enzi za JK
mikutano ya siasa yenye tija na maendeleo kwa jimbo haikatazwi.
 
Inaimarika kwa kudhoofisha wenzake?

Jambo la msingi kwa watawala ambalo wanapaswa kujiuliza kabla hawajatumia nguvu zaidi kutaka kuua upinzani ni hili:

Kwanini Mwl. Nyerere aliwakubalia wale wachache 20% na kuwanyima walio wengi 80% ambao ndio waliyakataa mageuzi?

Inapaswa watawala wafahamu kwamba Upinzani upo MOYONI na sio MACHONI

Hila na dhuluma hizi wanazowafanyia watanzania ni kuwalimbikizia HASIRA ndani ya mioyo yao na siku zitakapolipuka ndio tutajua kwamba MAGEUZI ndio mfumo wa kidunia HAYAEPUKIKI

Watawala fanyeni wajibu kwa haki msitumie hila.
 
Ila katika statement yako mwishon usisahau KWA MTUTU WA BUNDUKI usiliache hilo neno ni muhimu sana kwa mustakabali wa uimarikaji wa CCM mwaka 2017usiliache hilo kuliweka kwenye hoja yako.
 
Inatia faraja sana!inaleta ari ya kumshabikia na kumpambania Magufuli
Ujinga wenu huwa hauwaishi mnampambania magufuli?mnampambaniaje magufuli?kwa nini mnatumia nguvu nyingi sana kumpamba ? Maana nijuavyo mimi chema chajiuza chenyewe bila hata promotion! Mbona nawaona promotion zina zidi ? Au ndio sio chema ? Halafu tikiwaambia UVCCM wengi hamna akili mnanuna , mnaimarika kivipi wakati hampo kwenye ushindani?
 
Imeimarika ndio. Lakini kwa kuingia ulingoni na kumwelekeza refa kumfunga mikono bondia waliyenaye ulingoni. Hongereni sana
 
Hakuna demokrasia nzuri kama kuteua wapinzani katika nafasi za kiserikali.Hilo limefanyika mwaka huu
Hao wapinzan kina nani? Wapinzani makada watiifu?? Matawi yenu nayo ni wapinzani? Weken bunduki chini kwanza zipigane hoja hapo ndio tutaujua uwezo wenu na huko kuimarika mnako imba mmezuia watu kufanya siasa kwenye majimbo ya wengine halafu kina tulia wanashinda kugawa misaada kwenye majimbo ya wenzao wakati walio tenda kama wao walikamatwa!? Kweli CCM inaimarika kwa mtutu wa bunduki na utekaji nyaraa
 
mikutano ya siasa yenye tija na maendeleo kwa jimbo haikatazwi.
Kwahiyo katiba inaelekezaje mkuu au mnaikanyaga tu mjuavyo ninyi,

Je chama ca siasa kikifanya mikutano kwa ajili ya kujiimarisha ni kosa kubwa kwenu sio

Yaani mnapenda kusikia mnachokitaka tu sio
 
Hakuna aliyetarajia ikani ya ccm kutekelezwa vilivyo ndani ya muda mfupi hivi!

Huku kushuka kwa uchumi ni sehemu ya hiyo ilani? kwanini vitisho na hata matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya wanaosema ukweli dhidi ya awamu hi yameshamiri zaidi?
 

imefanikiwa na kuuwa nakuteka watu
 
Tumeimarika mnoo lakini kwa gharama kubwa sana..think and digest..Lakini tusijisahau upinzani huwa mioyoni mwa watu na sio kwa viongozi wao "wanaohamia" kwetu. Natamani 2018 tuwafungulie minyororo tuone wamakufa kiasi gani na kupima uimara wetu CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…