Aise kwa jinsi Lowassa anavyousaka urais inanikumbusha hadithi za alfuleulela mjini Bagdad Enzi za mfalme Harun Rashid, ati jamaa allijua katika mtaa ule kulukuwa na taa ya zamani yenye majini yake ni yeye tu alikuwa anajua matumizi yake, unajua kuipata hiyo taa akifanyanyaje, alinunua taa mpya 10 kama ile, akawa anapita nazo anaziuza akisema taa ee taa, taa mpya kwa taa kuukuu, akapata kuukuu moja
Kwenda mtaa wa pili akaletewa ile taa kuukuu yenye majin aliyokuwa anaitafuta, akamwambia yule aliyemletea chukua na hizi 8 zilizobaki
Sasa Mzee Lowassa kuna kitu anakitafuta kwenye huu urais, ana lengo nao maalumu, hilo lengo linaweza kuwa zuri au baya, so we can gamble.
Pia Lowassa akipata urais atakuwa amevunja ule usemi wa Kiswahili usemao "mkamia maji huwa hayanywi" basi yeye atayanywa.
For the first time in Tanzania history mtu kautafuta urais mithiri ya ng`ombe hakunywa maji jana sasa maji hayo kapewa leo.
KWA HIYO TUTAFAKARI TUSIFANYE MAMBO KIUSHABIKI.