Kisa: Nilivyowahi maishani

Umetisha Champ
 
Daah stori yako ni ya mateso sana. Aisee wanaume twapitia mengi
 
🙆
 
NAENDELEA PARTY 13

Sasa naanza nilipokuwa huko kwa ndugu yangu sana na si ndugu yangu tu pia alikuwa rafiki yangu sana yule mtoto wa aunt yangu...

Wakati naendelea kuumiza kichwa nitoke vipi huku nikiwa na ka akiba kangu nakatumia kwa nidhamu sana nilikuwa nanunua vitu siku ya mnada viazi vitamu kama vyote, unga dona kama wote, dagaa, magimbi, nyanya nk nilikuwa navyo vya kutosha geto.
Siku zilienda sn hatimaye ile hela ikawa imekata sasa niliteseka sn sjapata ona kulala njaa kushinda na njaa yote yangu ila ukiniona hata huwezi jua kama napitia hali ngumu ni mkimya tena naweza kukaa ndani peke yangu kimya na wala nisijskie vibaya kbs nikawa na amani tu.
Kwenda kule kwa ndugu yangu siwez sababu mkewe alikuwa jau sana nakumbuka nilipika ugari kisha nikaiwekea maji nikanawa ilikuwa asubuhi sa mchana nikashinda na njaa usku umefika A haikai wala B haikai ooooh niliamua kukomba ule ukoko wa maji machafu nikala aisee kisha nikalala tuli.

Siku zilisogea nilimpgia simu yule jamaa yangu mchungaji kwamba nataka kuja huko kwake akaseme niende maana pia alikuwa na ujenzi wa kanisa tasaidia, nilienda tukaanza fatilia kibali cha ujenzi nacho kikabuma watoa kibali walikataa sababu ya eneo.
So nikawa nipo nipo tu sasa hapo kwa jamaa yangu hakuwa mtu mbaya kabisa na ni moja ya rafiki zangu wakubwa sn wa pekee maana pia mi si mtu wa marafiki na makundi.
Nikiwa huko kwa rafiki yangu huyu ndugu yangu nikiyemuacha kagera akanipgia simu kwamba kanunua pool table kawapa watu wasimamie lakini hawampi hela kama vp nirudi anikabz mimi, daaah mi nikamwambia mbona staweza maana sjui lolote kuhusu mchezo huo akasema we njoo takuwa nakuja kukuonyesha.
Kweli niligeuza kagera na nikaanza simamia hilo pool taratibu nikaanza kujua kuchezesha na hatimaye akaniambia takuwa nampa elfu 50 kwa wiki zngne zote ni zangu nikamwambia sawa kazi ikaanza na kweli nilikuwa napata hela kiasi chake hela ya kula na kulipa kodi haikunikosa ila nilikuwa naangalia fursa zingne pale kwenye lile eneo.....

TAENDELEA
Niliingia kwenye mgogoro mkubwa sn na ndugu yangu baada ya mimi kuonekana napata maendeleo sana.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…