Kisa: Nilivyowahi maishani

NAENDELEA PARTY 8
Kwanza nirudi kwa yule dada J nini kilifanyika baada ya kuwa mm nimefukuzwa kazi kwasababu ya roho yake ya kwanini, kwani niliskia kwenye kikao akisema eti imekuaje mi naanza tu kazi nalipwa laki 4 wakatu yeye alianza kwa kujitolea tu kwanini na mimi nisijitolee kwanza.
Kumbuka hapo hata hajui mimi na mzungu tumetoana wapi anasahau pia mimi nilikuwa namzd elimu mbali sana maana yeye alikuwa na certificate tu ndo alikuwa anasaka diploma.
Aisee yule dada J alileta rafiki yake pale ofisini ndiye akawa mtu wa marketing na yeye J akarudi kukaa ofisini.
Ni kweli ambavyo nilinena haikupita hata miezi 2 naye akatimuliwa kwa kutia hasara kampuni yeye pamoja na shoga yake wakapgwa chini.

Haya turudi sasa baada ya kufukuzwa kazi sasa maisha yalikuaje kwa kifupi nilirudi kwenye msoto usio wa kawaida kabisa sikuwa na wa kunitia moyo maisha yangu yote, mama yangu alituacha tukiwa wadogo sana tumelelewa kimafungu mafungu tu yeye mama alirudi kwao huko akaolewa akasahau kabisa kuhusu watoto wake. ( Hii story taileta kivyake kuhusu mama na uhusiano wangu na mzee aisee watu wana roho mbaya sana ).
Ok nikiwa sina kazi rasmi sasa hapo mwanamke hajui kitu na niliapa sitamwambia maana nilijua akijua ataniongezea stress tu.
Kale ka hela nilikobakiza kama laki 2, nako siku 1 mchungaji akaniita kwake akaniomba niwaazime kanisani shs 150,000 baada ya wiki 1 itarudi nikasema hiyo sawa nikampa nikitegemea ni waaminifu itarudi mfukoni nikabaki na elfu 40 tu, wakuu skulipwa pesa yangu yaani skurudishiwa mpaka kesho alooo.

At last nilichafuliwa sana na mchungaji kwa washirika maana niliamua kuachana na mambo ya kanisani kabisa maana niliona kumbe hata hawa wachungaji nao ni walewale nikaamua jifunza kufanya meditation tu siyo mambo ya dini tena.

Msoto ulikuwa heavy skubadili ratiba ya kutoka home nilikuwa natoka kama kawaida alfajiri sn kama naenda kazini kumbe naenda town kutafuta kazi mwanamke ye anajua mi naenda kazni.
Mfumo huo nilienda nao karibu miezi 3 iliisha anaona tu mi natoka kwenda kazini kumbe wapi, akiniuliza salary namwambia kampuni imepigwa faini ya kodi hali si nzuri boss kasema tuvumilie atatulipa malimbukizo yetu.
Ikafikia hatua sasa ya kutembea sina kitu mfukoni naikumbuka na hela yangu niliyoazmwa daaah.
Nikawa natoka alfajiri natembea kwa mguu toka goba napita makongo juu to mlimani city mpaka mbezi stand nakanyaga tena mpk kkoo au naamua kuzuga zuga hapo mbezi stand kama nasubiri usafiri wa kwenda mahali kumbe mi na gain time tu muda usogee sogee naposema mbezi namaanisha stand ya mbezi kabla haijaamishiwa makumbusho enzi hzo.

Nilipgika viatu vikaisha, nguo zkachakaa sina wa kunisaidia wala kunionea huruma njaa yangu, jua langu, kiu yangu, joto langu.
Wakati mwngn naishia pale udsm nazama kwenye miti miti kule natafuta sehemu nakaa peke yangu nalia sana kimoyo moyo nafanya meditation mpk nasinzia huko aloooo alooooo...
Sasa nikaanza kuwa siku zingne nabaki home tu.
Je nn kilijili sasa nilipokuwa nikibaki home pale sku moja moja...

TAENDELEA....
 
Wanaume tunapitia shuruba nyingi sana, Mungu alituumba tuvunge tusiongee tu, right Kama tungekuwa na midomo mirefu ungejikuta wewe una afadhari
 
Ila, hivi kuanzisha family (ngono zembe) wakati hali ngumu hivyo inatokeaje hii Kiongozi?

Huyo binti hata kutaka kuondoka ni ugumu wa maisha tuu, msoto huu uwe mwenyewe, ukileta wategemezi inakuwa balaa mara mbili elfu.
Wakati wakaka wengine nasikia kwny maisha magumu hata mdudu hasimami na mwanadada haipitiki...
Ila kwa wengine ni sehemu ya kuapta faraja...
 
NAENDELEA PARTY 10

Nilikuwa sku zingine nabaki home
Niliamua kuwa napokuwa home najichimbia ndani kimya kabisa si rahisi mtu kujua kama nipo ndani labda mtoto akirudi shule si mnajua tena watoto baba baba nyingi sana.
Hili la kubaki home sku moja moja kumbe yule mwanamke akikutana mashoga zake wanaonijua akawa anawaambia yule jamaa leo atanikoma haiwezekani abaki home ngoja nirudi ajabu akirudi hata hasemi kitu ukzngatia pia mi si muongeaji na hajui hata naptia nn.
Mkumbuke hapo unakuta sjala chochote tokea asubuhi nilichokuwa nafanya ni kuhakikisha mtoto akirudi akute chochote ndani basi ila mimi tajijua sasa.
Maneno nikawa naletewa mengi sana na watu anayosema mwanamke ninayeishi naye ilifikia hatu akawa ananiambia nanuka sana maana yake hata kulala naye tu kitandani stakiwi maana anadai nanuka nyie acheni tu.
Nikifikilia nayoptia na haya maneno makali ya mwanamke nilikuwa naishiwa power kbs.

Kuna jamaa yangu mmoja nilimaliza naye chuo alikuwa kapata kazi ya kusimamia kiwanda cha kufyatua tofari maeneo ya goba ingawa kulikuwa na kaumbali toka hapo nilipokuwa siku zngne nilikuwa naenda huko nashinda huko kiwandani wakati mwngne napiga tofari nikirudi home nimechakaa mwili hoi maumivu kila kona lengo nipate ka hela ka kununua chochote kwaajili ya mtoto na mimi pia.

Siku zilisonga sioni kesho yangu kabisa, kuna ndugu yangu mmoja alinitafuta kwamba kuna taasisi mpya imeanzishwa kwaiyo nimekuwekea nafasi utakuja mwanza mmmmh nikasema angalau nimeanza ona nuru sasa.
Siku kadhaa zilipita akasema nitafute passport kubwa niwe nayo, nichome manjano, nichome corona kisha documents zote nizi scan nimtumie nilichakarika hasa kupata 150,000 ya passport mpka nikapata nikatuma vitu vyote alivyosema. Ila msoto uko palepale hakuna ahueni.
Nikawa namsumbua yule ndugu hiyo kazi vp majibu yakawa ni subiri takwambia tu daaah mara mwezi, mara miezi mara mwaka ukaisha story ni zilezile tu. Nilimtafuta jamaa yangu mmoja ni pastor alikuwa kanda ya ziwa huko nikamwambia nataka nije huko kwani kuna mchongo nauskilizia mwanza hapo akasema njoo bahati nzuri naye alikuwa ananikubali sana nilisoma naye A level na chuo nilisoma naye kimoja.
Nikasaka nauli mpaka nikaipata safari ya kuondoka dsm ikaanza mwanamke nakumbuka nilimwambia mi naondoka hapa ila starudi tena hapa nikamshukuru kwa yote na nikaondoka to kanda ya ziwa. Huku nyuma sasa yule mwanamke alikuwa akituma sms za kunitukana sn na kunikejeli madai yake ni hela ya mtoto daaaah kila nikijitetea lakini wp at last nilimwambia ampeleke home kwa mzee tarudi kumchukua hapo akagoma labda kama nataka chukua mtoto mpk nimuue kwanza yeye ndo nichukue mtoto.
Niliamua kubadili namba ya simu ili kuepuka maneno makali aliyokuwa akinitumia, nikiwa nipo kanda ya ziwa na jamaa yangu nili relax kdg akili ilifunguka sn na mwili ulirudi angalau nikawa mtu sasa.

TAENDELEA KUHUSU ILE KAZI YA NDUGU YANGU NI MAJANGA MATUPU...
 
Mkuu Kweli shida zinakupa upofu mpaka unamwambia mkeo ampleke mtoto kwa mzee wako(na mama yako wa kambo) ambao walikutimua kama mbwa koko? Ulitegemea huyo mtoto ataishije yani?
 
Mkuu Kweli shida zinakupa upofu mpaka unamwambia mkeo ampleke mtoto kwa mzee wako(na mama yako wa kambo) ambao walikutimua kama mbwa koko? Ulitegemea huyo mtoto ataishije yani?
We acha tu kuna matukio tawapa hapa khs huko kwa mzee ni noma sn raia hawa si ndugu si nani πŸ€”
 
Huyo mwanamke wako alikua alikua halipwi kwani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…