Kisa Dabi Basi la Timu la Chomwa Moto huko Libya

Kisa Dabi Basi la Timu la Chomwa Moto huko Libya

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mchezo wa Dabi nchini Libya kati ya Al-Ahli Tripol dhidi ya Al-Ittihad ulisimama katika dakika ya 39 baada ya Mashabiki wa Al-Ahli kuvamia uwanja kupinga goli la kutangulia la Al Ittihad.

Mwamuzi kutoka nchini Ureno Fábio José Costa, alijeruhiwa na mchezaji wa akiba na Mwamuzi akakataa kuendelea na mechi baada ya kutokea fujo ya mashabiki waliokuwa wanaonyesha kukataa goli hilo,

Wachezaji wa Al-Ittihad na wasimamizi wa mechi walilazimika kutoroka kwa usalama wao

Ghasia zilizuka ndani na nje ya uwanja.
Na Mashabiki wa Al-Ahli wakaamua kulichoma moto basi la timu ya Al-Ittihad na gari la polisi.
1750341492294.png

Chanzo: ManaraTv​
 
Maisha ya kimichezo hayahitaji kuwa serious hivyo.

Mwisho wa siku unashindwa kutumia utashi wako kufurahia mchezo na kujikuta unaongozwa na mihemko au siasa za michezo kama zile za Simba+Yanga ambazo mamlaka hutumia kuwahadaa wananchi wao na kuwatoa kwenye mambo ya msingi.
 
Back
Top Bottom