Kiprotokali Waziri akienguliwa akiwa katikati ya majukumu yake mikoani mambo gani husitishwa kwake mara moja?

Pia watu wa usalama wanaanza kukufwata zaidi maana sasa unakuwa subject watataka kujua reaction yako na ya watu wako wa karibu in and out nadhani ni hayo kwasasa
 
Hahaha mwigu bwana alishawahi mwambia mbuge flani unapoongea uwe unatahadhari ya kuwa unaongea na mtu aneyeongoza watu gani nyuma
 
Namba za kawaida anazipataje wakati mko safarini?
Gari zote za Majaji,Spika,Naibu Spika Mawaziri na Manaibu wake zina namba zake za usajili za serikali, STK,STL ama STJ....hivyo huwa zinavuliwa zinahifadhiwa kwenye gari humo humo ...ndio zinavalishwa namba za utambulisho wa vyeo......

Angalia post No.59
 
Iko hivi kiprotokali
1.mke anaanza kunawiri
2.NDUGU wanakoma kujisikia
3.wale mahawara wanatafuta chimbo jingine
4.walinzi na madereva wanashukuru,sala zao zimepokelewa
5.watoto wake ghafla kiburi kinakoma
6.x-waziri anaanza kusalimia hata watoto wadogo 'sikamoo'

7.Anaanza kujishaua na kujinyenyekeza kwa akina Lema,Mdee na Sugu

8.halafu anakacha kutinga mjengoni,hadi wenge LA kuwa 'backbencher' Lipoe

9.anaanza kupokea simu hata za tafadhali nipigie
 
DED.jpg
 
Ukiangalia hizo picha utagundua Waziri Kigwangalla wakati anateuliwa kuwa Waziri wa Utalii uteuzi ulimkuta akiwa njiani huko porini.

Wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Afya......ilibidi kibao cha Naibu waziri wa Afya Kung'olewa, bendera ishushwe iwekwe namba ya kawaida STL wakati huo akirudi ofisini kusubiri uapisho mpya

....kwa maana hiyo kila kitu kinaishia hapo hapo mara upatapo taarifa.

Nashukuru sana Mkuu kwa kunipa mfano hai, natamani maswali yote humu yangekuwa yanajibiwa kama ulivyofanya Mkuu, nadhani hii imelimisha wengi
 
atazitumia hizo kama nani

Namba zitaitambulisha gari kuwa ni ya serikali, mtumiaji anaweza kuwa mtanzania yeyote. Kuna magari mengi tu ya serikali yenye utambulisho wa namba STK /STL yanatumiwa na watu wasio mawaziri. Kwa hiyo kamakuna ulazima wa kurudi Dar/ Dom kwa gari hiyo ikiwa na namba hizo STK/STL ni sawa. Otherwise kama hataki bugutha na media attention , ataitisha gari yake personal ( I, belief kama mbunge ana gari yake binafsi) imfuate Kigoma au apande ndege
 
Ukiangalia hizo picha utagundua Waziri Kigwangalla wakati anateuliwa kuwa Waziri wa Utalii uteuzi ulimkuta akiwa njiani huko porini.

Wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Afya......ilibidi kibao cha Naibu waziri wa Afya Kung'olewa, bendera ishushwe iwekwe namba ya kawaida STL wakati huo akirudi ofisini kusubiri uapisho mpya

....kwa maana hiyo kila kitu kinaishia hapo hapo mara upatapo taarifa.View attachment 800660View attachment 800661
Umemaliza kilakitu hapa. Umeeleweka
 
Ni kuachia gari lirudi ofisini fastaa; hapo ni kupanda train ama basi ; bajaji au bodaboda kwenda kwako. Kesho ni fasta ofisini kwa HR kuchukua clearance form. Kama ulikopa benki mafao yako yote yanapelekwa huko ili mkamalizame vzr.

Kuachichwa kazi kunaumaa usiombe; kheri ummwage mwajiri wako kuliko akumwage wewe; hapo huwa ni timing principal.
 
Pia watu wa usalama wanaanza kukufwata zaidi maana sasa unakuwa subject watataka kujua reaction yako na ya watu wako wa karibu in and out nadhani ni hayo kwasasa
ooh,kumbe ndo maana Nape alionyeshwa mguu wa kuku na makofia,kwa kuhofia anaweza kusema visivyotakiwa kusemwa mwenye Presscon
 
Cha kwanza ukisikia taarifa za utenguzi wako, dereva wako anang'oa namba za Uwaziri zinawekwa za Kawaida.

Bendera inashuswa, hapo hapo unakuwa mbunge wa kawaida
Dereva anafanya hivyo kwa maagizo ya bosi wake au yy mwenyewe kwa kazi yake inavyosema?
 
Namba za kawaida anazipataje wakati mko safarini?
Gari ina namba mbili, ya uwaziri na stk.

Kile cha uwaziri kinakua kimefunika cha stk. Ikifika saa 12 jioni na yupo barabarani, kinaondolea na kinabaki cha stk. Bendera inashushwa.

Ikifika asubuhi kinawekwa juu ya stk
 
Gari zote za Majaji,Spika,Naibu Spika Mawaziri na Manaibu wake zina namba zake za usajili za serikali, STK,STL ama STJ....hivyo huwa zinavuliwa zinahifadhiwa kwenye gari humo humo ...ndio zinavalishwa namba za utambulisho wa vyeo......

Angalia post No.59
Umeeleweka vema mkuu
 
Back
Top Bottom