Kipindupindu ni Uchafu

Kipindupindu ni Uchafu

bartenderznz

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2016
Posts
398
Reaction score
195
Masika au Msimu wa mvua umepamba moto,sehemu kubwa ya Tanzania inanyesha,maeneo mengi kuna maji yaliyotuama na yanayotiririka.

Mito na mabwawa yamejaa,wakaa mabondeni nao wanataharuki,baadhi ya biashara haziendi ipasavyo.Kila kitu ni tirigivyoge hasa kwa wakaanzi wa mjini.

Pengine vijini Mambo shwari,yanasonga kwa kuwa jua lililowaka kwa siku 60 lilifanya mipunga isinyae mashambani sasa imenawiri na pengine kutunga mimba.

Kwa wakaanzi wa mijini nawasihi waendelee na ule utamaduni wao wa kuchemsha maji ya kunywa au kutumia ''water guad",tuwahimize watoto kunawa mikono kwa sabuni kila watokapo chooni n.k.

Masika bila kipindupindu inawezekana weka mazingira safi,safisha uwezavyo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom