Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 578
- 2,613
Ni ugonjwa wa kuhara unaosababishwa na maambukizi ya vimelea vya bakteria wanaoitwa Vibrio cholerae.
Vimelea hivi humwingia mtu kupitia matumizi ya vyakula au maji machafu yenye masalia yake, ambayo mara nyingi hutokana na kuchanganyikana na choo cha mtu mwenye ugonjwa huu.
Kipindupindu ni ugonjwa wa mlipuko, huhatarisha usalama wa afya ya jamii kwa ujumla, husambaa kwa kasi kubwa na huhitaji udhibiti na matibabu ya haraka ili kupunguza athari kwa mgonjwa pamoja na kuokoa uhai wake ili asiweze kupoteza maisha baada ya muda mfupi.
Dalili
Dalili zake huanza kuonekana kati ya saa 12 hadi siku 5 tangu vimelea vimpate mtu kwa mara ya kwanza. Baadhi yake ni hizi-
Matibabu
Mgonjwa hupaswa kufikishwa hospitalini haraka ili apate msaada. Kitendo chochote cha kumcheleweshea matibabu kinaweza kumfanya apoteze maisha.
Msingi wa matibabu ya ugonjwa huu huhusisha mambo matatu ya muhimu-
Kinga
Kwa asili yake, kipindupindu ni ugonjwa unaotokea kwenye jamii zisizotunza usafi, ni ugonjwa wa jamii chafu. Tunaweza kujikinga dhidi ya ugonjwa huu kwa kufanya mambo yafuatayo-
Chanzo: WHO/CDC/ STG NEMLIT 2021

- Kujisaidia choo chepesi kilichojaa maji (kuharisha maji)
- Kutapika
- Uchovu mkubwa
- Maumivu makali ya misuli
- Shinikizo dogo la damu
Matibabu
Mgonjwa hupaswa kufikishwa hospitalini haraka ili apate msaada. Kitendo chochote cha kumcheleweshea matibabu kinaweza kumfanya apoteze maisha.
Msingi wa matibabu ya ugonjwa huu huhusisha mambo matatu ya muhimu-
- Mgonjwa kuongezewa maji
- Matumizi ya dawa za viuavijasumu (Antibiotics/dawa za kupambana na bakteria)
- Matumizi ya madini ya zinc na asidi ya foliki (Folic acids)
Kinga
Kwa asili yake, kipindupindu ni ugonjwa unaotokea kwenye jamii zisizotunza usafi, ni ugonjwa wa jamii chafu. Tunaweza kujikinga dhidi ya ugonjwa huu kwa kufanya mambo yafuatayo-
- Tumia maji safi na salama kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika wakati wa kupiga mswaki, kwenye kunywa na unapokuwa unaandaa mlo wako.
- Kujisaidia chooni pekee. Tabia za kujisaidia vichakani au sehemu nyingine yoyote ile haifai. Aidha, usafi wa vyoo utunzwe.
- Kusafisha mikono kwa sabuni na maji tiririka baada ya kutoka chooni, wakati wa kuandaa chakula pia kabla ya kula
- Epuka ulaji wa chakula kibichi, pia kumbuka kuchemsha viporo
- Safisha vizuri matunda kabla ya kula
Chanzo: WHO/CDC/ STG NEMLIT 2021